Pages

Friday, February 6, 2015

NFT CONSULT WAPANIA KULETA MABADILIKO TANZANIA‏

DSC_0252
Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyoendeshwa na kampuni ya NFT Consult kwa maofisa rasilimali watu na watoa mafunzo kutoka makampuni mbalimbali nchini wakifanya usajili kabla ya kuanza kwa warsha hiyo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
MOJA ya makampuni makubwa yanayoshughulika na ushauri wa jinsi ya kuongeza ufanisi katika maeneo ya kazi, NFT Consult wameendesha kongamano kubwa la kutambua haja ya mahitaji ya wadau mbalimbali wa maendeleo hapa nchini.


Kampuni hiyo ya kimataifa ambayo imeingia nchini mwaka 2010 ikiwa na matawi Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini imesema kongamano hilo limelenga kuonesha uwezo wao katika kubadili mifumo ya utendaji kazi.
Ofisa Mtendaji wa kampuni hiyo, Badru Ntege amesema kwamba wamekuwa wakiendesha mafunzo mbalimbali yenye kueleza thamani ya mfanyakazi na mdau wowote ambapo uthamini wa wadau ndio unaotoa mwanya wa mabadiliko chanya yanayotakiwa
“Mafanikio ya eneo lolote lile linatokana na wadau kusikiliza wenzao na kisha kufanyia kazi kauli za upande wa pili.” Alisema Ntege.
DSC_0361
Timu ya NFT Consult ikijitambulisha kwa washiriki kabla ya kuanza warsha hiyo. Kutoka kushoto ni Inside Business Partner wa NFT Consult, Aisu Mori, Client Partner wa NFT Consult, Immaculate Mwaluko, Ofisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya NFT Consult, Badru Ntege, Meneja biashara mkazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania, Joan Ajilong na Client Partner wa NFT Consult, Sophia Shuma.
Alisema katika mafunzo ya kuthamini ,kanuni kubwa inayotumika ni kujipanga katika nafasi husika na kutumia changamoto kama fursa za kubadili mazingira ya kazi na kazi yenyewe ili kupata matokeo yanayotakiwa.
Alisema kwamba changamoto zinazotolewa na wadau katika kubadilisha mazingira yao ndio zinatumiwa na kampuni hiyo katika kuhakikisha makampuni na taasisi zinazotoa huduma zinazokidhi haja kwa muda unaotakiwa katika mazingira yanayobadilika kwa kasi.
Naye Meneja biashara mkazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania, Joan Ajilong akizungumzia shughuli wanazofanya alisema kwamba lengo kubwa ya warsha ya jana ni kuwaeleza wadau nini wanachoweza kuwapa ili wabadili mazingira yao ya kazi.
_DSC0594
Pichani juu na chini ni Ofisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya NFT Consult, Badru Ntege akitoa mada kuhusu mifumo saba ya kitabia katika utendaji wa kazi kwa maofisa rasilimali watu na watoa mafunzo kutoka makampuni mbalimbali nchini kwenye warsha ya siku moja iliyoratibiwa na kampuni ya JB's PR and Events.
Alisema watu wengi wamechoshwa na mazingira yale yale na kukata tama lakini kupitia mafunzo yao wamekuwa wakihakikisha kwamba wadau wanapata msukumo mpya wa kufanyakazi na kupata matokeo chanya kwa kasi.
Alisema kwamba tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo imefanikiwa kubadili wadau wao na kuanza kutambua kuthamini watu, kuwasikiliza na kujadiliana nao ili kupata matokeo yanayotakiwa.
Alisema kwa sasa NFT Consult imepata uzoefu na kufanyakazi katika nchi 6 za kusini mwa jangwa la sahara.
Nchi hizo ni Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.
Amesema mabadiliko makubwa katika namna ya kusimamia shughuli kunawezesha mabadiliko ya utendaji na kuleta ufanisi.
_DSC0585
Alisema kazi ya taasisi hiyo pamoja na kusaidia uwapo wa menejimenti na rasilimali watu zenye uhakika pia husaidia kupatikana kwa kada inayotakiwa kwa taasisi mbalimbali wakiombwa kufanya hivyo.
Nao washiriki kutoka TGNP waliohojiwa wakati wa mafunzo hayo walisema ipo haja kampuni hiyo ikaongea na watendaji wa serikali ili wakapatiwa mafunzo yatayogeuza changamoto kuwa fursa za kuleta tija katika uendeshaji wa serikali.
_DSC0672
Washiriki wakijaza chemsha bongo wakati warsha hiyo ya siku moja kwa maofisa rasilimali watu na watoa mafunzo kutoka makampuni mbalimbali nchini.
“Mafunzo haya yanawezesha kutambua ubora wa kuthamini na kuhakikisha unasikiliza kila mtu kwa ajili ya maendeleo, na changamoto za serikali mafunzo haya yanafaa sana kwao” alisema Shakila Maimana.
Alisema anaamini mafunzo hayo yanaweza kugeuza changamoto kuwa fursa za maendeleo.
Naye Diana Sembende alisema kwamba mafunzo hayo yamembadilisha na anaamini kwamba serikalini watumishi wanayahitaji sana.
_DSC0676
Kwa matukio zaidi ingia humu

No comments:

Post a Comment