Pages

Thursday, February 5, 2015

PICHA 3::HATIMAYE JUSTIN TIMBERLAKE ATHIBITISHA MKEWE KUWA MJAMZITO

BAADA ya kuwepo minong'ono ya hapa na pale kuwa mwigizaji Jessica Biel ana ujauzito wa mtoto wa kwanza wa mwanamuziki Justin Timberlake, huku mastaa hao wakikaa kimya, hatimaye staa Justin ameweka bayana kuwa mkewe huyo ni mjamzito.

Timberlake ameweka wazi hayo kwa kutupia picha katika mtandao wa Instagram jana ikiwa ni siku yake ya kuzaliwa akimbusu tumbo mkewe Jessica mwenye mimba na kuandika hivi:
'Namshukuru kila mtu aliyenitakia heri ya kuzaliwa! mwaka huu 



natarajia kupata zawadi kubwa mno. Nina hamu sana ya kumuona Mvulana au msichana  Huwezi kujua  Na sisi hatujui pia Wote tunasubiri kuona' aliandika Justin.

No comments:

Post a Comment