Matofali yaliyokuwa kwenye gari hilo yakiwa yamemwagika
chini.
WATU watano (5) wamenusurika kifo ajalini baada ya gari
walilokuwa wakisafirishia matofali kupasuka tairi la mbele na kuacha barabara
kisha kupinduka.
Ajali hiyo ilitokea jana jioni katika Kijiji cha Ng’ombe
wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza ambapo gari hilo aina ya Fuso lenye namba za
usajili T726BMY mali ya Sanne Shimbe, lilikuwa likiendeshwa na tajiri huyo.
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo, gari hilo lilikuwa
kasi, tairi ikapasuka hivyo gari likapoteza uelekeo na kuacha barabara kisha
kupinduka.
“Gari lilikuwa kasi hivyo baada ya tairi kupasuka lilitoka
barabarani na kuingia kwenye matuta ya viazi vitamu likakwama ndipo
likapinduka,” alisema shuhuda.
Kwa upande wake dereva Shimbe, alisema baada ya tairi
kupasuka alijitahidi kulizuia gari hilo lisianguke lakini ilishindikana.
“Nilijitahidi kuliweka sawa gari barabarani baada ya tairi
kupasuka lakini ilishindikana kabisa ndio likatoka barabarani na kupinduka
lakini nashukuru Mungu tumetoka wazima.
“Tulikuwa watano, mmoja wetu ndiyo ameumia mguu na
ameshapelekwa hospitali, anaendelea vizuri, sisi wengine hatukupata majeraha,”
alisema Shimbe.
No comments:
Post a Comment