Wanafunzi
wa shule ya Sekondari Ilala, iliyopo Karakata Jijini Dar es Salaam
wakiandamana jana kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kufikisha
kilio chao cha kubomolewa uzio wao na wananchi wanaoizunguka shule hiyo.
Wanafunzi hao
Wanafunzi
hao wakiandamana na kufunga barabara ya Nyerere, Mandela na Uhuru kwa
muda wakati wakipita kwenda Ofisi ya Mkoa wa Mkoa.
Wanafunzi
hao wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo. Ambapo
hata hivyo, Mkuu wa Mkoa walipishana nae njiani kwani alikwenda shuleni
kwao kusikiliza kero yao.
wanafunzi hao walisema kuwa kiliochao hasa ni kutokana na uongozi wa shule kuwachangisha shilingi 20,000/= kila mmoja kwaajili ya ujenzi wa uzio huo uliovinjwa juzi jioni baada ya wao kutoka shule.
Amri ya kubomolewa kwa ukuta huo inadaiwa kutolewa na Mwenyekiti
wa Serikali za Mtaa huo, Greyson Maliki kinyume cha sheria
sio cha kiungwana kwani pamoja na kwamba kulikuwa na mgogoro wa muda
mrefu katika eneo hilo, bado shule hiyo ina wanafunzi wa eneo hilo na wazazi
wao wamelipia katika ujenzi wa ukuta.
Mwenyekiti huyo, Afisa Mtendaji wa Kata
na Mjumbe wa mtaa huo wameshikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano.
Ulinzi mkali ofisi ya Mkuu wa Mkoa.Picha na Father Kidevu Blog
No comments:
Post a Comment