Robot inayo msaidia Cole
Mwanafunzi mmoja katika mji wa Pennsylvania nchini Marekani
alipata ajali ya gari na kuumia vibaya na sasa anahudhuria masomo kwa msaada wa
njia ya roboti.
Cole Fritz alikuwa alikuwa hawezi kuhudhuria masomo yake
mara baada ya ajali mwezi mmoja uliopita,lakini kwa sasa anaouwezo wa
kufuatilia kila kinachoendelea kwa msaada wa roboti.
Pennsylvania ilikodisha kifaa hicho kutoka katika
kampuni
inayotoa mafunzo ya namna ya kutumia roboti hizo katika mitandao ya
kijamii.Kimsingi kifaa hicho ni sawa na iPad ambayo imeinuliwa juu vya
kutosha.Naye Cole huwa anakiendesha kifaa hicho kupitia kinakilishi chake na
vitufe vya kubofyea kitu ambacho yeye anakielezea kuwa sawa na kifaa cha
michezo ya kinakilishi ya runinga.ana sema Roboti hiyo inamsaidia kufuatilia
masomo yake bila taabu yoyote na pia awapo shuleni anakutana na marafiki zake .
Ni vyema na furaha kubwa kuonana na kila mmoja niliye mzoea
na kuzungumza nao.
Wakuu wa shule anakosoma Cole wanasema roboti hiyo
inawasaidia kupunguza gharama za mwanafunzi huyo.na wanajaribu kuzungumza kuwa
hawajui ingekuwaje kwa mwanafunzi huyo bila kifaa hicho,pengine ingewalazimu
kumpeleka mwalimu kila siku nyumbani kwa akina Cole kumfundisha,lakini roboti
hiyo inamsaidia Cole kupata elimu bora,kwa kumpa maelekezo kupitia waalimu wake
kama kawaida na roboti hiyo imekuwa sehemu ya darasa la Cole.
Kwa muujibu wa maelezo ya Cole, roboti hiyo si sanifu sana
lakini si haba ni mwanzo mzuri na maendeleo yako wazi mbele yake.
Madaktari wanaofuatilia afya ya kijana huyo ,wanasema kwamba
Cole atarejea shuleni akiwa hali ya kawaida mapema mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment