Pages

Thursday, February 5, 2015

TAARIFA::JESHI LA POLISI LAZUIA MAANDAMANO YA UVCCM YALIYOKUWA YAFANYIKE



 Na Chalila Kibuda 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imezuia maandamano ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Ilala (UVCCM) ya kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa chama hicho pamoja na kuacha kiporo  maandamano ya Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha).

Akizungumza Jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ,Kamishina wa Jeshi la Polisi ,Suleiman Kova ,amesema kuzuia kwa maandamano hayo inatokana na kuwepo kwa taarifa za Kiintelejensia za kuvuruga amani.

Kova amesema maandamano ya UVCCM Wilaya ya Ilala yalitakiwa kufanyika kesho lakini kutokana na kuwepo kwa taarifa za kiintelejensia za Machinga ,Bodaboda ,Mama Lishe na Baba Lishe kushiriki maandamano na kufikisha malalamiko yao kupitia maandamano hayo.




Amesema kumekuwepo kwa taarifa katika mitandao ya jamii wakihamasishana bodaboda na machinga ,mama lishe na baba lishe kushiriki maandamano pamoja na kutoa ujumbe wao kwa kupitia maandamano katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Kova amesema machinga ,Mama lishe,Baba,na Bodaboda watumie taratibu zingine za  kufikisha ujumbe kutokana na sheria zilizowekwa na sio kutumia mgongo katika vyama vya siasa.

Kwa upande  Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) maandamano yao yalikuwa yanahusu kwenda tume ya Taifa ya Uchaguzi ni lini itaanza kuandikisha daftari la wapiga kura ,pamoja na wanafunzi watashiriki vipi upigaji kura ambapo Kamanda Kova amesema hilo wanaweka kiporo kwanza wanafanya uchunguzi wa taarifa mbalimbali.

“Sisi tunachoangalia amani kwani maandamano ya amani yanaweza kufanyika lakini mwisho wa siku inakuwa sio amani kwa jeshi la polisi tunawajibu kuangalia hilo”amesema Kamanda Kova.

CHANZO: MICHUZI BLOG

No comments:

Post a Comment