Serikali imetakiwa kukamilisha haraka mchakato wa
kutoa posho ya mazingira magumu kwa walimu wanaofanya kazi katika
mazingira magumu ili kuwafanya walimu waipende kazi yao na kuendelea
kufanya kazi maeneo ya pembezoni.
Mwenyekiti wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Magreth
Sitta, alitoa wito huo jana wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji
wa shughuli za
kamati yake bungeni jana.
kamati yake bungeni jana.
Alisema idadi kubwa ya walimu wanaoteuliwa kwenda kufundisha katika
maeneo ya pembezoni ama hawaendi kabisa au wanapokwenda hawaka kwa muda
mrefu kutokana na mazingira hayo kutokuwa rafiki.
Alisema ili kukabiliana na hali hiyo umefika wakati ambao sasa
Serikali ikamilishe mchakato wa kutoa posho ya mazingira magumu kwa
walimu hao ikiwa kama motisha wa kuwafanya wasiondoke kwenye mazingira
yao ya kazi.
“Ili kuimarisha utoaji wa elimu hususan katika maeneo ya pembezoni,
Serikali ikamilishe mapema iwezekanavyo mchakato wa kutoa posho ya
mazingira magumu kwa walimu wanaofanya kazi katika mazingira magumu ili
kuwafanya wabaki kazingira ya kazi ikiwamo kuipenda kazi yao,” alisema
Sitta.
Aidha, aliitaka Serikali kuweka mkakati wa makusudi wa kuboresha
mazingira ya utoaji elimu kwa watu wenye mahitaji maalum kwa kutenga
fedha za kutosha kwenye sekta hiyo.
Sitta alisema kuwa katika mkakati huo, Serikali pia itoe mwongozo
wa kitaifa kuhusu ujenzi wa miundombinu ya shule na vyuo na kutaka
usajili wa shule na vyuo hivyo uzingatie mahitaji ya kundi la watu wenye
mahitaji maalum.
Katika mapendekezo ya Kamati yake, Sitta pia aliitaka Serikali
kukabiliana na ongezeko la vyuo vinavyotoa elimu ya ufundi bila
kuzingatia vigezo vilivyowekwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
(Nacte).
No comments:
Post a Comment