Rais wa Gambia
Waendesha mashtaka nchini Marekani wamewafungulia mashtaka
raia wa tatu wa Marekani kwa kuhusika kwenye njama ya mapinduzi nchini Gambia.
Alagie Barrow aliye na uraia wa Marekani na Gambia
alifikishwa mahakamani kwenye jimbo la Minnesota akikabiliwa na mashtaka ya
kuendesha harakati za kijeshi dhidi ya nchi rafiki.
Taarifa ya mahakama ilisema kuwa bwana Barrow alishukiwa
kusaidia kupanga mapinduzi hayo.
Mapinduzi hayo yalifeli wakati walinzi wa rais
walipowafyatulia risasi wale waliojaribu kuendesha mapinduzi hayo ambayo
baadaye walisafiri kwenda nchini Marekani ambapo walikamatwa.
No comments:
Post a Comment