Mashabiki wanadai kuwa mamlaka zilisababisha vurumai
zilizotokea baada ya kufungua lango moja pekee
Misri imesimamisha kwa muda usiojulikana ligi kuu ya nchi
hiyo baada ya watu zaidi ya Watu 20 kufariki dunia.
Kati ya waliofariki ni wengi wao ni Mashabiki wa timu ya
Zamalek ambao walifariki kutokana na msongamano wakati Polisi walipowafyatulia
mabomu ya machozi baadhi ya mashabiki waliokuwa wakijaribu kuingia kwa nguvu
ndani ya uwanja wakati timu hiyo ilipokuwa ikipambana na timu ya ENPPI.
Mtandao mmoja nchini humo uitwao AL-Misriyun umeripoti.Tukio
hilo limetokea baada ya Polisi kutumia gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha
mashabiki walikokuwa wakitumia nguvu kujaribu kuingia uwanjani.
Taarifa ya Wizara ya mambo ya ndani ya Misri inasema kuwa
Mashabiki wa Zamalek walikuwa wanataka kuingia uwanjani kwa nguvu hivyo
walikuwa wakiwazuia ili kunusuru mali ya uma isiharibike.
Polisi wamesema mashabiki hao walikuwa wanataka kuingia
uwanjani bila tiketi, wamenukuliwa wakisema Watu hao walipoteza maisha baadhi
kutokana na msongamano mkubwa wengine walipokuwa wakipambana na Polisi.
Ndani ya uwanja kulionekana rundo la viatu karibu na miili
ya Watu waliopoteza maisha na wengine waliolala wakiwa majeruhi.
Mashabiki wa Zamalek wanadai kuwa vurumai zilianza mamlaka
ya uwanja ilipofungua Geti la waya kuwaruhusu kuingia ndani.
Mashuhuda wanasema uzio ulianguka wakati Watu walipokuwa
wakipigania kuingia ndani hali iliyosababisha msongamano mkubwa, mara askari wa
usalama walianza kurusha mabomu ya kutoa machozi.
Watu walianza kukanyagana hali iliyosababisha Watu kupoteza
maisha.
Tukio hili limetokea ikiwa ni miaka mitatu tangu Wapenzi wa
soka zaidi ya 70 walipopoteza maisha wakati vurugu zilipotokea katika uwanja wa
ndege wa Port Said.
Baada ya tukio hilo idadi maalum iliwekwa kwa
watakaohudhuria Mechi kwa hofu ya hali ya usalama ,inaelezwa kuwa mipaka hiyo
iliyoondolewa hivi karibuni huwenda ikawekwa tena baada ya tukio la mwishoni
mwa juma lililopita.
No comments:
Post a Comment