Katibu Mwenezi akizungumza na waandishi wa habari jana, katika Makao Makuu ya Chama hicho.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha,Isaack Joseph akizungumza
na waandishi wa habari jana katika makao makuu ya chama hicho na kudai
kushangazwa na kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape
Nnauye ya
kuwa makundi yanayokwenda nyumbani kwa Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, kumshawishi kugombea Urais kuwa na kusema kuwa makundi hayo yanachokifanya ni utekelezaji wa kauli ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa katika sherehe za CCM mjini Songea, alipowaruhusu watu wakawashawishi wanaoona wanafaa kuwania nafasi mbalimbali.(Habari Picha na http://jamiiblog.co.tz/
kuwa makundi yanayokwenda nyumbani kwa Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, kumshawishi kugombea Urais kuwa na kusema kuwa makundi hayo yanachokifanya ni utekelezaji wa kauli ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa katika sherehe za CCM mjini Songea, alipowaruhusu watu wakawashawishi wanaoona wanafaa kuwania nafasi mbalimbali.(Habari Picha na http://jamiiblog.co.tz/
Katibu
Mwenezi akifafanua kuhusu kauli ya Nape na kusema “Rais alisema kama
mnafikiri kuna watu wanaofaa kugombea Urais, muwafate mkawaombe, sasa
napata shida kidogo sielewi watu kwenda kwa Lowasa, sijui anapoteza sifa
ipi ya kuwania Urais, sioni kosa la ukiukwaji wa Kanuni, siyo vizuri
kubishana na kauli ya kiongozi wako, lakini kauli hiyo kidogo hata mimi
kama Mwanachama wa CCM ilinitisha”alisema Isaack Joseph
Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM),Mkoa wa Arusha, Robinson Meitinyiku,
akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa Habari, ambapo amekitaka
Chama hicho kusimamia misingi, katiba na kanuni kwa wanachama na
kukaripia wote wanaofanya makosa na kumtaka Nape kuheshimu na kutambua
maadili ya utu na kumtaka atambue kuwa Lowasa ana watu nyuma yake
ambao wanampenda, kumheshimu na kumjali, hivyo UVCCM hawatakaa kimya
kuwasemea wanyonge wanaokwenda kumshawishi Lowasa agombee..hapo
akifafanua Katiba ya CCM inavyowapa wanachama fursa ya kuwaona viongozi
wao.
Katibu huyo akiendelea kufafanua jambo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari.
Kulia
ni Mwandishi wa habari wa Kituo cha Radio5,Arusha Mohamed na kushoto ni
Grace Macha wa Tanzania Daima, wakifuatilia mkutano huo.
Muonekano
katika ofisi ya Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha,waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali hapa nchini wakifuatilia mkutano huo.
Na Pamela Mollel,Arusha
Chama
Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Arusha kimesema hakipingani na makundi
yoyote yanayokwenda kumshawishi Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu
Mstaafu, Edward Lowasa kuchukua fomu ya kuwania urais katika uchaguzi
Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu na kusema kuwa Sauti
ya watu ni Sauti ya Mungu.
Aidha
Umoja wa Vijana wa CCM(Uvccm) mkoani hapa kimedai kushangazwa na
kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye,ya kudai kuwa
kitendo cha makundi ya watu wanaokwenda nyumbani kwa Lowasa kumshawishi
agombee Urasi, hakumwondolei Lowasa sifa za kuwania urais kwa kuwa
hakuna kipengele kwenye Katiba au Kanuni ya CCM kinachokataza wanacahama
kufata viongozi.
Hayo
yalisemwa jana jijini hapa na Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM mkoani
hapa,Isaack Joseph alipokwua akizungumza na waandishi wa habari katika
makao makuu ya chama hicho na kusema kuwa kimeshangazwa na kauli ya
Nnauye kwani kinachofanyika ni utekelezaji wa kauli ya Rais Jakaya
Kikwete aliyoitoa katika sherehe za CCM mjini Songea alipowaruhusu watu
wakawashawishi wanaoona wanafaa kuwania urais.
Alisema
kwamba kwa tabia na mila za kiafrika mtu akitembelewa na mgeni hana
budi kumkaribisha ,kumkirimu pamoja na kumfanyia maandalizi yote na
kusema kuwa makundi mbalimbali yameona Lowasa anafaa ndio maana
yamekwenda kumshawishi agombee.
“Kama
kuna makundi yanayomfuata Lowasa na yaende kwani Sauti ya watu ndio
sauti ya Mungu watu wameona anafaa ndio maana wamemfuata kumshawishi
sasa kunamuondoleaje sifa?”alihoji Joseph
Hatahivyo,alisema
kuwa Lowasa tangu apewe adhabu ndani ya chama hicho hakuwahi kuongea
lolote na hata baada ya kufunguliwa adhabu hiyo baadhi ya makundi
yamekuwa yakimfuata kwa kuona anafaa na kumtaka Nnauye kuacha kuropoka
hovyo.
Kwa
upande mwenyekiti wa UVCCM mkoani Arusha, Robinson Meitinyiku
alimshangaa Nnauye kwa kauli yake kwa kuwa katiba ya chama hicho ibara
ya 14 inamruhusu mwanachama yoyote kumtembelea kiongozi wake kwa kufuata
taratibu.
Alisema
kuwa kuna baadhi ya makundi ambayo yamekuwa yakiwashawishi baadhi ya
makada wa CCM na hata wengine kutoa sadaka na vitabu kuwanadi wagombea
wao lakini hawakemewi zaidi ya Lowasa,jambo linaloonyesha Nape kuegemea
upande mmoja.
Alimtahadharisha
Nnauye kwamba Lowasa ni kiongozi mkubwa hapa nchini na ana wafuasi
wengi nyuma yake hivyo hata wao wakiona anafaa kugombea Urais na
wakipata fursa ya wkenda kumtembelea na kumshawishi wataenda.
“Lowasa
ana watu wengi nyuma yake tunamheshimu na sisi kama vijana wa Arusha
tuna haki zote kumtetea tutamfuata hivi karibuni kumshawishi agombee
hatuwezi kukaa kimya kwa kuwa tunaona anafaa”alisema Meitinyiku
No comments:
Post a Comment