Kama Umeifuatilia na kuiangali Video ya Fid Q Bongo Hip-Hop
Kupitia Account ya Director Nisher kwenye Youtube Basi utakuwa Shahidi kuwa
Video hiyo Iliondolewa na Wamiliki wa YouTube Kitu ambacho watu wamekitafsiri
Tofauti.
Taarifa za Mtaani watu wamesema eti Imefungiwa na Kampuni
Flani South Africa baada ya Nisher kucopy Vitu flani kwenye Video yao.
Fid Q amefunguka ukweli kupitia Kipindi cha DUNDO cha
MamboJamboRadio Arusha na kusema kuwa sababu za Video hiyo Kutolewa ni sababu
yeye Fid Q amejiandikisha kabisa na anatambulika ndani ya YouTube na kuilinda
Hatimiliki ya Fid Q Wao kama Youtube Wameiondoa wakidhani kuwa Nisher ni
Mdananda wakati wao Wameshamuuliza Fid Q kama Video aliyoipost kwenye Account
yake ya Cheusi Dawa Ni yeye na alivyowajibu ndipo Wakafungia ya Nisher bila wao
Kujua kama Nisher pia anahusika kwenye HatiMiliki ya hiyo Video akiwa kama Director.
Hiyo ndiyo sababu Fid Q alomweleza @DjHaazu kuwa ndiyo issue
iliyopelekea Video hiyo Kuzuiliwa kwa Masaa Kadhaa kupitia account ya Nisher
No comments:
Post a Comment