Shirika
la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia
wakazi wa KIMARA na TABATA; Miji ya Kibaha na Mlandizi mkoani Pwani
kuwa, tangu Jumapili ya Tarehe 01/03/2015 Mtambo wa kuzalisha Maji wa
Ruvu Juu umepata hitilafu baada ya bomba la Majighafi (Raw-Water)
kuachia kwenye moja ya chemba ya kuchukulia Maji eneo la Mtamboni.
Hali hii imelazimu kuzima Mtambo wa Ruvu Juu.
Mafundi
wa DAWASCO wanaendelea na matengenezo ili kuhakikisha Huduma ya Maji
inarejea katika hali ya kawaida ifikapo siku ya Ijumaa 06/03/2015.
Wakazi
wa maeneo yafuatayo wameathirika na hitilafu hii; MLANDIZI, KIBAHA,
KIBAMBA, MBEZI, KIMARA, UBUNGO, CHUOKIKUU, KIBANGU, RIVERSIDE, BARABARA
YA MANDELA, TABATA, NA SEGEREA.
KWA TAARIFA ZAIDI PIGA SIMU KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NAMBA 022 5500 240-4 au 0658-198889
DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU AMBAO NI WA DHARULA.
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
“DAWASCO TUTAKUFIKIA |
No comments:
Post a Comment