Pages

Wednesday, March 18, 2015

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYA YA LONGIDO


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Longido Ndugu Michael Lekule Laizer mara baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Engikareti mpakani mwa wilaya ya Arumeru na Longido.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza wimbo maalum kutoka kwa wenyeji waliokuja kumpokea wa kijiji cha Engikareti.

 
Loishiro Yaseya Katibu kata ya Engikareti wilaya ya Longido akisoma risala mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo walimuelezea tatizo kubwa ni ugomvi wa mipaka na wilaya ya Arumeru.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Engikareti waliokuja kumpokea mpakani mwa wilaya ya Longido na Arumeru.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa vazi la kimila la heshima na wananchi wa Kijiji cha Engikareti wilaya Longido.

Mkuu wa Wilaya ya Longido Ndugu Ernest Kahindi akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Engikareti wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza wimbo wa mapokezi alipowasili kwenye kijiji cha Longido kata ya Longido ambapo aliweka jiwe la msingi katika jengo la hoteli ya kisasa ya mfugaji Ndugu Kitasho Simel Nakutamba.

Mzee Kitasho Simel Nakutamba akimpa mkono Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika hoteli yake ya hapo Longido

Jengo la kisasa linalojengwa kwa ajili ya Hotel na mfugaji Kitasho Simel Nakutamba

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na vijana wa kimasai alipowasili  kwenye kituo cha mafunzo Learning In Longido .

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi kwenye majengo ya kituo cha mafunzo cha Learning In Longido.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata mapokezi ya aina yake alipowasili kwenye kijiji cha Ketumbeine ambapo alitembelea mradi wa ufugaji wa ng'ombe madume bora ya mbegu.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiandaa sindano ya chanjo tayari kwa kumchoma ng'ombe.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kumchoma ng'ombe chanjo kwenye mradi wa ufugaji wa madume bora katika kijiji cha Ketumbeine.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kwenye kijiji cha Ketumbeine mara baada ya kushiriki kuchoma chanjo za ng'ombe.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa jengo la hoteli katika kijiji cha Kitumbeine,kulia ni mmiliki wa hoteli hiyo Ndugu Halifa Juma.
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Lesingeita ambapo alishiriki ujenzi wa nyumba ya watumishi wa Afya.

Bendera ya Chama Cha Mapinduzi ikipepea kwa masaa 24 kwenye kijiji cha Lesingeita karibu na mradi wa wananchi wa kujenga nyumba za watumishi wa kituo afya.
Katibu wa Kikundi cha akina mama cha Msanja Flora Kaaya akisoma risala kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Kikundi hicho kinajishughulisha na ufugaji wa mbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua bendera tayari kuipandisha kwenye shina la wakereketwa wa Madereva wa Noah na Hiace pamoja na wafanya biashara ndogo ndogo Namanga
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Eworendeke ambapo alimpongeza mbunge wa jimbo la Longido kwa uamuzi wake wa kutogombea uchaguzi ujao na kusema wanasiasa wengi wanajua kuingia kwenye siasa lakini wakisahingia hawajui wakati gani wa kutoka.
 Wananchi wakifuatilia hotuba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Eworendeke ambapo alisema ni makosa makubwa kwa wanaowania nafasi za kugombea  kupita pita kabla ya wakati rasmi kwani kunapunguza ufanisi wa viongozi waliopo madarakani.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Eworendeke ambapo alitoa salaam za shukrani kwa CCM wilaya ya Longido kwa kuipa ushindi mzuri wakati wa uchaguzi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi na bendera za laiyekuwa Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Longido ambaye amejiunga na CCM kwenye mkutano uliofanyika Eworendeke.
 Wananchi wakisikiliza hotuba kwa makini.
 Mbunge wa Jimbo la Longido Mh.Michael Lekule Laizer akihutubia wananchi wa Eworendeke ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa hatogombea kwenye uchaguzi ujao wa Oktoba 2015.

No comments:

Post a Comment