Sylvester Marsh, enzi za uhai wake akiteta jambo na kocha
aliyewahi kuinoa Taifa Stars, Kim Poulsen
Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa
Taifa Stars Sylvester Marsh amefariki dunia jana alfajiri katika
Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kocha huyo aliyefanya kazi na makocha mbalimbali wa kigeni
alifariki dunia wakati akihudhuria kliniki ya ugonjwa uliokuwa ukimsumbua wa
saratani ya koo.
Familia ya Marsh ilisema hali ya kocha huyo ilibadilika
ghafla siku tatu zilizopita kabla ya mauti hayajamkuta.
Itakumbukwa kwamba Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF)
Jamal Malinzi alipoingia madarakani alibadilisha uongozi ikiwemo kuondoa benchi
la ufundi.
Marsh ndiye kocha wa kwanza kuipandisha Azam FC ligi kuu
Tanzania Bara mwaka 2007, pia amewahi kuzipandisha ligi kuu Toto Africans
(1998), Geita Gold Mines na Kagera Sugar.
Enzi za uchezaji wake dimbani alikuwa nafasi ya mlinzi wa
kati, akizitumikia Coop United, JKT, Mzizima, RTC Kagera, Polisi Mara, Tusker
FC (Kenya) na Iganga Town Council (Uganda)
Alizaliwa mwaka 1957, hadi mauti yanamkuta alikuwa na kituo
cha michezo Marsh Athletes Centre jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment