Jimbo la Mbarali kama yalivyo mengine lilianza
siasa za vyama vingi mwaka 1995 kwa ushawishi wa kipekee kutoka kwa
vyama mbalimbali, huku NCCR Mageuzi ikionyesha kila aina ya makeke.
CCM haikuwa na hofu na ilimtumia kiongozi mzoefu
wa kijeshi, Kanali Mstaafu Edmund Mjengwa ambaye hakufanya ajizi,
aliwashinda wapinzani na kutunza heshima ya CCM hapa Mbarali. Kanali
Mjengwa aliongoza kipindi kimoja, 1995 -2000.
Mwaka 2000 katika Uchaguzi Mkuu, CCM ilibadilisha
ladha na kumleta mwanamama. Huyu ni mtaalamu wa masuala ya uhasibu,
Estherina Kilasi.
Estherina alivaa viatu vya kanali mstaafu kwenye
kampeni na ni kama alijengewa ujasiri wa kijeshi, hakuwaogopa wanaume na
akasaidiwa na mtandao wa CCM ambao kipindi cha nyuma ulikuwa na maana
ya ushindi.
Alitangazwa mshindi na akafanikiwa kuongoza Jimbo la Mbarali kwa kipindi cha kwanza mwaka 2000 – 2005.
Mwaka 2005 unakumbukwa kwa kimbunga cha Kikwete
pamoja na matokeo yenye utata kwa maana ya upigaji kura uliokuwa
umepitiliza, (siku za mbele katika uchambuzi wa masuala ya siasa
tutakuja kuongelea masuala ya kushuka na kupanda kwa upigaji kura ambako
kunatia shaka).
Wapigakura walijitokeza kwelikweli na kazi kubwa
ikafanywa na wagombea huku CCM wakimpa nafasi mwanamama Estherina ambaye
alikuwa ameongoza kipindi kimoja.
Vyama vya CUF na TLP vilikuwa na nguvu jimboni humu na kufanikiwa kuweka wagombea, ule utitiri wa vyama wa mwaka 1995 ulipotea.
Filimbi ya upigaji kura ilipopulizwa na matokeo
kutangazwa, mwanamama Estherina aliwabwaga wagombea wa TLP na CUF.
Estherina alipata kura 52,713 akifuatiwa na Pwilla Getrudi Jacob wa TLP
kura 10,168 na Kharid Shaweji wa CUF kura 6,912.
Kwa jumla vyama vya upinzani vilijitahidi a lakini
viliangushwa na dhana ya ushindi wa kimbunga wa CCM katika kila kona ya
nchi. Bi Estherina akawa na ridhaa mkononi na akawa mtumishi wa wananchi
hadi mwaka 2010.
Mwaka 2010 ulifika huku vyama vikiwa vimejiimarisha na CCM ikiendelea kutumia juhudi za mtandao wake.
No comments:
Post a Comment