Mafuriko nchini Madagascar yamewaua watu 14
Watu 14 wameuawa kwenye mafuriko nchini Madagascar ambapo
pia wengine 20,000 wamelazimika kuhama makwao.
Mafuriko hayo yaliukumba mji mkuu Antananarivo na maeneo
yaliyo karibu.
Utawala unasema kuwa mvua nyingi siku zijazo huenda
ikasababisha madhara zaidi.
Mvua kubwa imenyesha nchini humo kwa takriban wiki mbili.
Mwezi uliopita kimbunga Chedza kiliwaua watu 80 nchini
Madagascar.
No comments:
Post a Comment