Gari aina ya Toyota Hilux ambayo imegongwa na Basi la Kampuni ya Majinja likiwa linatoka Mbeya kwenda Dar. |
Mtu
mmoja amefariki dunia na wengine zaidi ya 40 wamenusurika kifo katika
ajali ya barabarani iliyotokea majira ya saa 12:15 asubuhi njia panda ya
Mafiati jijini Mbeya ikihusisha magari mawili yaliyogongana uso kwa
USO.
Ajali
hiyo imehusisha basi la abiria mali ya kampuni ya Majinja lililokuwa
likielekea Dar es Salaam kutoka jijini Mbeya na gari dogo ambalo
halikufahamika Mara Moja.
kutokana na kuharibika sana ambalo dereva wake amepoteza maisha pale pale na hakufahamika jina lake mara moja.
Pamoja
na hayo shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mlinzi katika kituo cha Oilcom
Mafiati amesema kuwa dereva wa basi la Majinja ambaye hakufahamika kwa
jina alikuwa akiendesha gari kwa mwendo kasi kitu kilicho sababisha gari
kumshinda na kuparamia gari do go lililokuwa likitokea Mwanjerwa na
kuharibika kabisa.
Taarifa
tuliyoipata katika eneo la tukio ni kwamba hakuna abiria yeyote
aliyejeruhiwa kutoka katika basi hilo la abiria na mwili wa marehemu
ulichukuliwa na askari kwaajili ya uchunguzi zaidi.
CREDIT TO FAHARI NEWS |
No comments:
Post a Comment