Ajali hii imehusisha magari manne ambayo ni busi la Super Shem lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, Land cruiser ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, Canter na Mistubish. Ajali hii imetokea eneo la Undomo kata ya Uchama wilayani Nzega.
Watu 09 wamejeruhiwa na watu 06 waliokuwemo kwenye Land Cruiser mali ya Serikali ya Halmashauri ya Wilaya ambao kati ya hao 05 wanne ni watumishi wa Serikali walifariki dunia papo hapo. Magari yote manne yameharibika vibaya sana, canter iligongana na mistubish na bus liligongana na land cruiser ambayo imeharibika vibaya sana, imechanika kama scrapper.
Ajali ilitokea majira kati ya saa 3:30-4:00 usiku. Majeruhi 09 wapo hospitali ya Wilaya na maiti 05 zipo mochwari hospitali ya Wilaya(Nzega). Kwa mujibu wa Mganga mganga mkuu wa hospitali ya Nzega amethibitisha Kutokea kwa ajali hiyo.
TASAF, UNICEF WAZINDUA MPANGO WA STAWISHA MAISHA KUNUSURU KAYA MASIKINI
DHIDI YA UTAPIAMLO
-
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SERIKALI kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF)kwa kushirikiana na
wadau wa maendeleo na hasa Shirika la Kimataifa la Kuhu...
34 minutes ago
No comments:
Post a Comment