Pichani ni Aliyekuwa Mlinzi wa Dokta Slaa,Bwana Khalid Kagenziakuzingumza na Waandishi wa Habari mda huu
Pichani Mlinzi wa Kagenzi akionyesha mateso aliyofanyiwa na
Makada wa Chadema
SIKU chache kupita baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema. Mabere Marandu kufichua njama za Mlinzi
wa Katibu Mkuu wa Chama hicho Wilbroad Slaa, bwana Khalid Kangezi
kupanga-
Katibu Mkuu wa Chama hicho Wilbroad Slaa, bwana Khalid
Kangezi kupanga-
Mipango ya kumuua katibu huyo huku akishirikiana na Vigogo
wa Chama Mapinduzi CCM pamoja na Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa
Kinondoni,naye Mlinzi huyo bwana Kagenzi ameibuka kufichua siri nzito ndani ya
Chama hicho kikuu cha upinzani nchini.Anaandika KAROLI VINSENT Endelea nayo
hapo.
Akifichua siri hiyo Mda huu Jijini Dar es Salaam Mbele ya
Waandishi wa Habari amesema anasikitika sana na madai ya uongo yanayoenezwa na
viongozi wa Chadema huku wakifacha ukweli wa Mambo kwani ukweli way eye
kuzushiwa uongo huo unatokana na kuwa na mahusiano na Mke wa Dokta Slaa .
“Leo nashangaa sana hawa Viongozi hawa wa Chadema wanaosema
mimi ni nimehusika katika mipango ya kumuua Slaa,wanaficha ukweli kwani sababu
yote hii ya kuzushiwa uongo inatokana na mimi kuwa na mahusiano mabaya na Mke
wa Slaa,nilipoenda kumwabia Slaa”
“na akasema niende kumalizana na mke wake lakini ukweli na
mke wake mambo hayakwenda vizuli ndipo hapo Slaa akapeleka kwenye uongozi wa
juu”amesema kagenzi.
Akionyesha Vidonda
Mlinzi Kagenzi ameongeza Mala baada ya Dokta Slaa kupeleka
ugomvi huo kwenye ngazi za juu,ndipo yeye siko moja anakuja ofisini akakamatwa
na kupelekwa kwenye chumba cha utesaji ambacho anadai kinamilikiwa na chama
hicho.
Bwana Kagenzi ameendeleo kusema kuwa hata madai wanayodai kwamba
anahusiano wa karibu
na usalama wa Taifa pamoja na Vigogo wa CCM anadai ni ya
uongo mkubwa kwani hana mahusiano na watu hao.
“Jamani hivi inaingia akilini kweli mimi leo na maisha yangu
haya niwe na uhusiano na watu wa usalama na CCM,huu ni uwongo wa hali ya juu.na
wanataka kunichafua kwa jamii,tena niseme ukweli chama hiki kinataka kuficha
ukweli juu ya mambo waliyonitendea.”
“Ni kwamba mimi nimekuwa mlinzi wa dokta slaa kwa mda wa
miaka mingi sana ,tena mimi nilikuwa nampikia na kumtengea hadi chai ya kunywa
eti leo niambiwe naandaa mipango ya kumuua huo ni unafiki”amesema Kagenzi
Katika Jambo la kushangaza Mlinzi huyo amefuchua mipango ya
kitesaji na kigaidi inayofanya na Chadema huku akisema wameandaa ofisi ya
utesaji.
“Jamini hiki chama ambacho kinandoto ya kuchukua nchi leo
kinaandaa mipango ya mauaji na utesaji kama walivyonifanyia maana wameniteka na
kunifungia kwenye chumba cha utesaji wanachomiliki wao wamechoma visu.na kuweka
kwenye Mashine ya umeme bila kosa lolote,eti wakinishinikiza mimi nitaje
wanaonituma,jamani nawaambia mimi anitumi mtu”ameedelea kusema Kagenzi.
Aidha,Kagenzi amekitupia lawama chama hicho huku akisema
kwenye mateso waliyomtesa yamemfanya apoteze hata nguvu za kiume .
Alibanisha kuwa hata alivyokuwa mlinzi wa Dokta Slaa kwa
miaka mitano zaidi alikuwa analipwa malipo madogo ya Laki tatu kwa mwezi lakini
anasema kuwa hakuandaa mipango ya yoyote ya kumuua,lakini anashangaa kwanini
leo wanamsingizia kiasi hicho kwani amedai kuwa kama angekuwa anataka kufanya
vitendo vya kukisaliti chama angefanya huko nyuma.
Kuhusu kuingiziwa Milioni saba kwenye simu yake na watu wa
Usalama wa Taifa.
Kagenzi amesema hizo ni taarifa za uongo zinazosemwa kwani
hata simu yake haina salio ya pesa na haijawai kupokea pesa hizo.
Hatua anachukua.
Kagenzi amesema hatua iliyopaki sasa hivi ni kwamba tayari
ameshahojiwa na jeshi la Polisi na kilichobaki sahivi ni kusubili kesi
mahakamani,ili kukishtaki chama hicho kwa Vitendo walivomfanyia navyodai ni vya
kiuwaji.
No comments:
Post a Comment