Pages

Tuesday, March 10, 2015

TAARIFA KUHUSU SHAHIDI WA MAKAMU WA RAIS WA KENYA

Makamu wa Rais Kenya, William Ruto ndani ya Mahakama ya ICC.
Serikali ya Kenya imeutambua rasmi mwili wa mtu mmoja uliopatikana katika mbuga ya wanyama ya Tsavo, kuwa ni wa Meshack Yebei ambaye alikuwa shahidi katika kesi inayomkabili makamu wa rais wa Kenya William Ruto. kwenye Mahakama ya ICC.Mkemia wa serikali ya Kenya ametangaza kuwa mwili huo ambao ulikuwa umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti tangu mwezi December mwaka 2014 ni wa Meshack baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi wa chembechembe za DNA.
Meshack Yebei
Meshack Yebei alitekwa mwishoni mwa mwezi December nyumbani kwake 



Eldoret alipokwenda kumwona mkewe aliyekuwa anaumwa, familia yake ililalamika kuwa kutoweka kwa Yebei kunatokana na kuhusishwa na kesi hiyo.
Yebei alitarajiwa kuwa shahidi wa Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto kwenye kesi yake ya mauaji inayoendelea Mahakama ya ICC, The Hague.
Marehemu alipewa nafasi ya kupata ulinzi na makazi salama lakini akakataa, Serikali ya Kenya itafanya uchunguzi kugundua kilichosababisha kifo chake.

No comments:

Post a Comment