Leo tarehe 30/03/2015 waandishi wa habari walifika kituo Kikuu
cha Polisi wakitaka kujua uhalali wa silaha iliyokamatwa tarehe
29/03/2015. Silaha hiyo ni Bastola aina ya BERRETA yenye
namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu. Pia zilikamatwa risasi 17 za
Short Gun.
Ufafanuzu ni kama ifuatavyo:
Uchunguzi wa kina na wa kitaalam sasa umethibitisha kwamba
silaha hiyo inamilikiwa kihalali na Askofu Josephat Gwajima.
Kuhusu risasi 17 za Short Gun ni kwamba Askofu Gwajima
anamiliki Bunduki aina ya Short Gun yenye namba 102837
ambayo inatumia risasi za aina ya hizo zilizokamatwa.
Kuhusu watu 15 wanaotuhumiwa kujaribu kumtorosha Askofu
Josephat Gwajima bado uchunguzi unaendelea. Aidha watu hao
pia wanahojiwa kuhusu suala la kukutwa na silaha na risasi
zilizotajwa hapo juu wakati wao sio wamiliki halali za silaha hiyo
na risasi hizo na idadi iliyotajwa kwa mujibu wa sheria.
Baada ya uchunguzi wa suala hilo jalada la kesi litapelekwa kwa
mwanasheria wa Serikali kabla hawajafikishwa mahakamani ili
sheria ichukue mkondo wake.
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
S. H. KOVA,
DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment