Naomi Peter akitoa kipondo kwa mumewe.
Wawili hao wakazi wa Misheni, jijini Mwanza waliibua
timbwili la aina yake ambalo liliwavuta watu wengi chanzo kikiwa ni mwanaume
huyo kumkataa mtoto aliyezaa na mwanamke huyo.
“Siku ya tukio, Naomi alimpeleka mtoto wake nyumbani kwa
mzazi mwenzake kutokana na kutopewa hela ya matumizi, wakati huo Shila alikuwa
na mwanamke wake mpya ndani, baada ya mabishano ya muda ndipo Naomi akaanza
kumshughulikia Shila kwa kumtandika mangumi.
“Jamaa alikuwa hapeleki matumizi kwa mzazi mwenzie, mbaya
zaidi alikataa na kudai mtoto si wake ndipo timbwili lilipoanzia,’’ kilisema
chanzo hicho.
...Atimaye kipondo kikiendelea.
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, wakati ugomvi huo
ukiendelea mwanamke wa John wa sasa alikuwa kimya ndani na kushuhudia mpenzi
wake akipokea kichapo kisha kumkabidhi mwanaye amlee na yeye akaondoka zake.
Hadi shuhuda wa habari hizi anaondoka eneo la tukio, muafaka
juu ya kilichofikiwa ulikuwa bado haujapatikana.
No comments:
Post a Comment