Pages

Monday, April 20, 2015

Afariki kwa kugongwa na treni Morogoro


Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kugongwa vibaya na treni wakati akivuka reli na kisha viungo vyake kusambaa katika mtaa wa ujenzi manispaa ya morogoro .
Wakizungumza na ITV mashuhuda wa tukio hilo wamesema marehemu alijulikana kwa jina moja la mangi ambapo wameeleza kusikitishwa na ajali kwakua hii ni mara ya tatu watu kugongwa na treni katika maeneo hayo na kueleza kuwa amarehemu alikua anavuka Reli.

 
Naye mwenyekiti wa mtaa wa ujenzi Christopha Chales ameelezea tukio hilo na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kupita kwenye njia ya Reli kwani wataendelea kusababisha ajali zisizo za lazima ambazo zingeweza kuepukika.
Askari wajeshi la polisi wamefika katika eneo la tukio na kuchukua mwili wa marehemu ambapo umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa morogoro

No comments:

Post a Comment