Meneja wa Manchester United Louis van Gaal anadhani klabu
hiyo itamteua Ryan Giggs kuchukua nafasi yake. Giggs alikuwa meneja wa muda na
kusimamia mechi nne msimu uliopita baada ya David Moyes kutimuliwa. Aliteuliwa
kuwa meneja msaidizi wa Van Gaal mwezi Mey mwaka jana. Van Gaal, 63, anakaribia
mwisho wa msimu wake wa kwanza na mkataba wake unakwenda hadi mwaka 2017.
Alipoulizwa kuhusu Giggs, ameiambia TV ya Man United- MUTV: "Natarajia
kuwa atakuwa meneja mimi nitakapoondoka." Ameongeza kusema: "Sasa
mimi nina majukumu yote. Yeye ana jukumu kama la wachezaji. Kila anachokifanya
kwangu mimi anakifanya vyema sana." Giggs, 41, amesema ulikuwa "muda
wa kujivunia" katika fani yake wakati alipokuwa meneja wa muda, kufuatia
kufukuzwa kwa Moyes. Giggs, aliyeichezea Manchester United mara 963, alishinda
mechi mbili, kutoka sare moja na kupoteza mechi moja, wakati akiwa meneja wa
muda.
No comments:
Post a Comment