Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic
amefungiwa kucheza mechi nne za ligi kuu ya Ufaransa baada ya kunaswa na picha
za televisheni akitukana.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Sweden alikasirika na
kuwashutumu waamuzi na pia kutukana baada ya timu yake kupoteza 3-2 dhidi ya
Bordeaux mwezi uliopita. Ibrahimovic, 33, baadaye aliomba radhi na kusema
matamshi yake "hayakuwa yamelenga Ufaransa au wananchi wake".
Atakosa mechi nne kati ya saba zilizosalia za ligi. Kamati
ya nidhamu ilisema adhabu hiyo imezingatia "aina ya kosa na uzito wa
matamshi yake".
Ibrahimovic pia atakosa mchezo wa kwanza wa robo fainali ya
Champions League dhidi ya Barcelona kufuatia kadi nyekundu aliyopewa katika
mchezo uliopita dhidi ya Chelsea. Hata hivyo ataweza kucheza mechi ya fainali
ya kombe la ligi siku ya Jumamosi dhidi ya Bastia.
No comments:
Post a Comment