Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa
kushirikiana na Polisi Mkoa wa Pwani linaendesha oparesheni kali ya aina yake
ya kuwasaka majambazi waliowavamia, kuwaua askari wawili na kumjeruhi mmoja na
kisha kupora bunduki aina ya SMG.
Tukio hilo limetokea tarehe 30/03/2015 majira ya saa mbili
usiku huko barabara ya Kilwa Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Katika
tukio hilo majambazI wapatao 8 hadi 10 wakiwa na
mapanga na silaha
zingine waliwavamia ghafla askari watatu waliokuwa kazini katika eneo la
kizuizi cha Polisi kilichopo kijiji cha Kipara mpakani Kata ya Vikindu Wilaya
ya Mkuranga Mkoa wa Pwani. Majambazi hao waliwashambulia ghafla askari hao
kisha kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30 ndani ya magazine na
kutokomea kusikojulikana.
Majina ya askari wa Wilaya ya Kipolisi ya Mbagala waliouawa
ni kama ifuatavyo:
D.2865 SGT FRANCIS,
E.177 CPL MICHAEL,Askari mwenye namba D5573 D/SGT ALLY
amejeruhiwa kwa risasi kwenye paja la mguu wa kushoto na amelazwa katika
hospitali ya Temeke kwa matibabu. Askari huyu kabla ya kujeruhiwa alipambana
vikali na majambazi hayo kwa kutumia bunduki aliyokuwa nayo aina ya SMG ambayo
walishindwa kumpora hivyo wakatokomea kuelekea porila Vikindu.
Katika oparesheni hiyo, nguvu na mbinu zote za kipolisi
zitatumika ambapo vikosi vya Dar es Salaam na Pwani vilianza kufanya oparesheni
hiyo mara baada ya tukio ili kuhakikisha kwamba majambazi hao wanapatikana
haraka iwezekanavyo.
Pamoja na oparesheni hiyo kali inayoendelea, Jeshi la Polisi
linachunguza ili kubaini kama tukio hili linaashiria vitendo vya ugaidi au ni
ujambazi wa kutumia silaha.
Natoa wito kwa wananchi wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam
kupitia (dhana ya polisi jamii) kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa hali na
mali kwa kutoa taarifa sahihi.
IMETOLEWA NA:
S.H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM
No comments:
Post a Comment