Borussia Dortmund wamethibitisha kuwa Jurgen Klopp ataondoka
katika klabu hiyo ya Bundesliga mwishoni mwa msimu. Klopp, 47, ameomba
kukatisha mkataba wake ambao ulikuwa unakwenda hadi mwaka 2018. Ameifundisha
Dortmund tangu mwaka 2008 na kushinda makombe mawili ya ligi na
kucheza fainali
ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2012-13. Lakini msimu huu timu hiyo ilikuwa mkiani
mwezi Januari kabla ya kupanda hadi nafasi ya kumi, wakiwa pointi 37 nyuma ya
Bayern Munich wanaoongoza ligi. Kocha huyo amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa
vya England, ikiwemo Manchester United kabla ya kuteuliwa kwa Louis van Gaal,
Arsenal wakati ikisuasua, na baadaye mabingwa watetezi Manchester City, ambao
wamporomoka hadi nafasi ya nne, pointi 12 nyuma ya Chelsea wanaoongoza ligi.
No comments:
Post a Comment