Picha za waathirika wa shambulio hilo wapatao mia moja na
arobaini na nane ziliwekwa bayana katika ibada ya mkesha, katika maadhimisho ya
kuhitimisha maombolezo ya kitaifa nchini humo yaliyodumu kwa muda wa siku tatu.
Ni huzuni,kupoteza wapendwa wangali wachanga.
Kulikuwa na kaburi la muda,misalaba na mishumaa vilivyowekwa
katika viwanja vya mji mkuu wa Kenya ,Nairobi ili kuwakumbuka wanafunzi
waliouawa katika shambulio la chuo kikuu cha Garissa ,shambulio ambalo
lililotekelezwa na mwanamgambo aliyekuwa na silaha kutoka katika kundi la Al
Shabaab,mwishoni mwa wiki iliyopita.
Waandaji wa mkesha huo waliwataka waombolezaji waliokuwa
tayari kuhudhuria ibada hiyo, kuvaa mavazi meusi,na pia kubeba maua ridi .
Mapema,wanachuo kutoka chuo cha Garissa waliandamana katika mji mkuu wa
Nairobi,huku wakiwa na ujumbe wenye kuitaka serikali ya Kenya kuimarisha ulinzi
nchini humo.
Garissa kwenyewe watu wapatao elfu mbili walikusanyika
katika mkutano wa hadhara ,nayo mahakama kuu mjini Nairobi imetoa mwezi mmoja
zaidi kwa polisi kuwahoji washukiwa sita wa tukio la Garissa ambao wanashukiwa
kuwapelekea silaha wauaji waliotekeleza tukio lile.
No comments:
Post a Comment