Hatimaye mdau wa muziki nchini Tanzania ambaye ni Mwanzilishi na aliyewahi kuwa Meneja wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Shaban Taletale 'Abdul Bonge' amezikwa leo Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro.
Abdul Bonge enzi za Uhai wake
Mamia ya waombolezaji wakiwemo wanamuziki Diamond Platnumz, Dully Sykes, Shetta, Shilole, Dogo Janja, Profesa J, Quick Racka na wengineo wameshiriki mazishi ya Abdul Bonge.
Abdul Bonge alifariki dunia jioni ya Machi 28 mwaka huu baada ya kuanguka alipokwenda kusuluhisha ugomvi wa rafiki yake maeneo ya Magomeni-Kagera jijini Dar es Salaam-Picha zote na Dustan Shekidele, GPL, Morogoro
Maziko ya Mwanzilishi na aliyewahi kuwa Meneja wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge yakifanyika leo kijijini kwao Mkuyuni, Matombo mkoani Morogoro.
Mwili wa Abdul Bonge ukiombewa kabla ya maziko leo.
Wanamuziki mbalimbali wakiwemo Shetta, Diamond Platnumz, Profesa J, Quick Racka wakishiriki maziko ya Abdul Bonge.
Mwili wa Abdul Bonge ukitolewa ndani kupelekwa eneo la kuombewa.
Mdogo wa marehemu Abdul Bonge ambaye ni Meneja wa Mwanamuziki Diamond Platnumz, Hamisi Shaban ‘Bab Tale’ akilia wa simanzi juu ya jeneza lenye mwili wa mdogo wake.
Babu Tale akiwa na majonzi baada ya mwili wa mdogo wake kutolewa nje.
Waombolezaji wakijaribu kumtuliza Bab Tale.
Wanamuziki Shilole (kushoto), Madee (katikati) wakiwa na Meneja wa TMK Wanaume Family, Yamoto Band na Diamond, Said Fella wakati wa mazishi ya Abdul Bonge leo mkoani Morogoro.
Wanamuziki Dully Sykes, Diamond Platnumz na Shetta wakiwa katika mazishi ya Abdul Bonge leo.
Diamond Platinumz akiwa kwenye mazishi ya Abdu Bonge Mkoani Morogoro leo.
Diamond Platinum Ameongozana na Mpenzi wake Zari the Big boss kwenye Mazishi ya Aliyekuwa Mwanzilishi wa Kundi la Tip top Marehemu Abdul Bonge Aliyefariki juzi
Malunde1 blog inatoa pole kwa wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Abdul Bonge kwa msiba huu uliotokea.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU ABDUL BONGE MAHALI PEMA PEPONI. AMEN.


No comments:
Post a Comment