Mwanamke
akiwa hajitambui ndani ya gari la polisi baada ya kudaiwa kubakwa na
wanaume zaidi ya saba( tumeficha sura kwa sababu ya maadili)-picha zote
na Veronica Natalis
Chumba kinachodaiwa kutumika kufanya unyama huo |
Nyumba ya mama Seni |
Wananchi wakiwa eneo la tukio |
Baadhi ya watu waliokamatwa na polisi wakipandishwa kwenye gari la polisi |
Mama Seni akipandishwa garini - Picha zote na Veronica Natalis |
Kuna stori zingine ukizisikia unaweza kufikiri ni utani ama ndoto!!
Hii ya leo imetokea mkoani Shinyanga,ambapo
Mwanamke mmoja ambaye anasadikiwa kuwa
mkazi wa mtaa wa Matanda katika manispaa ya Shinyanga amefanyiwa vitendo
vinavyoelezwa kuwa ni ubakaji na wanaume saba tofauti hali iliyosababisha
kupoteza fahamu.
Tukio hilo limetokea leo katika mtaa wa Tambukareli kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga katika nyumba ya mama
aliyefahamika kwa jina la mama Seni ambaye anajihusisha na biashara ya kuuza
pombe za kienyeji.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwanamke huyo ni miongoni mwa wateja wa pombe za kienyeji
waliofika kwa mama Seni na baada ya kulewa alianza kuvutwa na wanaume ambao pia
ni wateja waliokuwa wamelewa.
Wamesema kutokana na hali hiyo ilimlazimu mwenye nyumba
ambaye ndiye muuzaji wa pombe za kienyeji kumuingiza mwanamke huyo chumbani
pamoja na wanaume waliokuwa wanamvuta ambao ni zaidi ya 7 .
"Huku
kwenye pombe hakuna adabu kabisa,unaambiwa miongoni mwa waliombaka wamo
vijana wenye nguvu ,watanashati zaidi ya saba,basi wakamfanyia ukatili
,tunaomba jeshi la polisi litende haki,waliotenda ukatili wapo na
wanajulikana kabisa,tunataka wachukuliwa hatua za kisheria",mashuhuda
waliongeza.
Mwenyekiti wa mtaa wa Tambukareli Roja Mshana amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na ametowa wito wa wananchi hasa wanawake kujiepusha na
unywaji wa pombe wa kupindukia ili kuzuia vitendo vya ukatili kwa wanawake
vinavyoendelea kutokea.
Mwandishi wa habari hizi amefika eneo la
tukio na kushuhudia gari la
polisi likiwachukua wanaume watatu wateja wa pombe za kienyeji, muuzaji wa
pombe hizo aliyehafamika kwa jina la mama Seni
pamoja na mwanamke aliyefanyiwa vitendo hivyo ambaye inasadikiwa kuwa
alikuwa amepoteza fahamu.
No comments:
Post a Comment