Mkude akiwa ameshikilia msalaba wa baba yake katika makaburi
ya Kinondoni jijini Dar jana jioni.
Mkude akiweka shada la maua baada ya mazishi ya baba yake
katika Makaburi ya Kinondoni, Dar.
Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ akiweka
shada ya maua katika kaburi la mzee Gerald Mkude ambaye ni baba mzazi wa kiungo
wa Simba, Jonas Mkude, jana jijini Dar.
Kiungo wa Simba, Abdi Banda (wa pili kushoto) akiwa na
waombolezaji wengine katika msiba wa mzee Gerald Mkude ambaye ni baba mzazi wa
kiungo mwenzake wa Simba, Jonas Mkude.
Kiungo wa Simba Jonas Mkude akiwa na majonzi wakati
akisikiliza misa ya ibada katika msiba wa baba yake mzee Gerald Mkude,
Konondoni jijini Dar.
Makamu wa Rais wa Simba, Kaburu akimfariji Jonas Mkude
katika msiba wa baba yake, nyumbani kwao, Kinondoni Studio jijini Dar.
Viongozi wa Simba, kutoka kushoto: Frisch Colins, Kaburu na
Ally Suru wakiwa katika Makaburi ya Kinondoni kufuatilia mazishi ya baba mzazi
wa kiungo wa timu hiyo, Jonas Mkude.
MZEE Gerald Jonas Mkude ambaye ni baba mzazi wa kiungo
mkabaji wa Simba, Jonas Mkude amezikwa leo Jumanne jioni katika Makaburi ya
Kinondoni jijini Dar, baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo tangu Novemba
mwaka jana.
Mzee huyo ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 46,
alilazwa katika Hospitali ya Mwananyamala tangu Alhamisi ya wiki iliyopita
kabla ya Jumapili kufariki akiwa katika hospitali hiyo ya Mkoa wa Kitabibu wa
Kinondoni.
Bwana ametoa na bwana ametwaa na jina lihimidiwe, amina.
(PICHA: NASSOR GALLU/ GPL)
No comments:
Post a Comment