Baadhi
ya vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kutoka wilaya
za Nyamagana, Magu, Busega na Bunda wameanza matembezi ya siku sita
kuelekea katika kijiji cha Butiama kwenye kaburi la hayati baba wa taifa
Mwalimu Julius Nyerere kwa lengo la kuwahamasisha watanzania kujitokeza
kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa
ajili ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani unaotarajia
kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Matembezi
haya ya vijana wa Chadema yameanzia eneo la igoma jijini Mwanza, mahali
ambako mwaka 1967, Mwalimu Julius Kambarage
nyerere aliishia baada ya kutembea kwa miguu kutoka mwitongo, Butiama mkoani Mara akiunga mkono azimio la Arusha.
nyerere aliishia baada ya kutembea kwa miguu kutoka mwitongo, Butiama mkoani Mara akiunga mkono azimio la Arusha.
Kiongozi
wa msafara huo George Charles ambaye ni mwenyekiti wa baraza la vijana
wa Chadema (Bavicha) kata ya igoma anasema lengo la matembezi hayo ya
zaidi ya kilometa 260 pamoja na mambo mengine ni kupinga ufisadi, mauaji
ya watu wenye ulemavu wa ngozi – Albino, vikundi vya kihalifu
vilivyoibuka jijini Dar es Salaam maarufu kama panya road, ambapo
wamelitaka jeshi la polisi kutowazuia na safari yao kwa vile matembezi
hayo ni ya amani kwa ajili ya kumuenzi baba wa taifa.
Baadhi
ya vijana wanaoshiriki matembezi hayo wanasema wameamua kufanya hivyo
kwa dhamira njema ili kuwahamasisha watanzania kujitokeza kujiandikisha
na pia kupinga uporaji wa raslimali za taifa unaodaiwa kufanywa na
baadhi ya watu wachache waliokabidhiwa dhamana ya uongozi na kusababisha
ufa mkubwa kati ya wenye nacho na wasionacho huku wananchi walio wengi
wakiendelea kukabiliwa na umaskini.
No comments:
Post a Comment