Rand Paul seneta wa Kentucky
Seneta kutoka Kentucky wa chama cha Republican Rand Paul,
ametangaza nia rasmi, kuwa atagombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao
nchini Marekani.
Paul ameyasema hayo wakati wa kampeni zake anazoziendesha
kupitia tovuti yake, na amenukuliwa kuwa anataka kuirejesha nchi hiyo katika
kanuni uhuru na serikali ndogo.
Kampeni zake alizindulia katika jimbo la Louisville mapema
wiki hii. Rand Paul ameungana na seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz, katika
harakati hizo ambazo zimevuta hisia za nusu ya
wagombea wakubwa wa chama cha
Republican,na hii ni pamoja na gavana wa zamani wa jimbo la Florida Jeb
Bush,gavana wa Wesconsin Scott Walker,ambaye bado hajatoa tamko lake rasmi .BBC
No comments:
Post a Comment