Baadhi ya wanafunzi waliokuwa chuoni hapo.
Shambulio hilo linadaiwa kufanyika mapema leo wakati waumini
wa dini ya Kiislamu wakiwa katika sala yao ya alfajiri.
Watu walioshuhudia tukio hilo wameeleza kuwa kuna majeruhi
wengi ndani ya chuo hicho.
Wapiganaji hao wanadaiwa kuwa ndani ya chuo hicho mpaka sasa
wakiwa wamewateka nyara watu kadhaa huku Jeshi la Kenya na maofisa wa polisi
wakiwa tayari katika eneo la tukio kukabiliana na watu hao.
Mpaka sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lililokiri
kutekeleza shambulio hilo japo Kundi la Wapiganaji wa Somalia, Al Shabaab
likihusishwa kufanya shambulio hilo.
No comments:
Post a Comment