Pages

Friday, April 10, 2015

SKYLIGHT BAND YAZIDI KUPASUA ANGA NA MUZIKI WA LIVE, NJOO USHUHUDIE LEO THAI VILLAGE‏

DSC_0616
Aneth Kushaba AK 47(katikati) akiimba na waimbaji wenzake wa bendi ya Skylight ambao ni Ashura Kitenge(kushoto) na kulia ni John Music kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba na kucheza moja ya Sebene la Kikongo pamoja Sony Masamba.
 
Sony Masamba ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na waimbaji wenzake kulia ni Sam Mapenzi na kushoto ni Joniko Flower
Waimbaji wa Skylight Band wakiimba kwa moja ya nyimbo za bendi yao kwenye kiota cha Thai Village ijumaa iliyopita.
Sugua sugua mpaka itakate......Waimbaji wa Skylight Band wakicheza moja ya style zao zinazobamba mujini.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiimba sambamba na msanii mwenzake Sam Mapenzi kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Burudani ikiendelea kutolewa na wasanii wa Skylight Band.
Ashura Kitenge akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band huku akisindikizwa na Aneth Kushaba AK 47(kushoto) pamoja na John Music (kulia)
Ashura Kitenge akiimba kwa hisia pamoja na Sam Mapenzi mbele ya mashabiki wa Skylight Band(hawapo pichani) kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Sugua Sugua mpaka utakate njoo leo ujifunze kusugua kama hawa mashabiki wa Skylight walivyojua mmoja ya Style ya kusugua
Sam Mapenzi akiendelea kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight band (hawapo pichani) huku akisaidiwa na waimbaji wenzake wa kwanza kushoto ni Ashura Kitenge akiwa smambamba na Sony Masamba(wa pili kutoka kushoto) pamoja na John Music (wa kwanza kulia) kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Ni mwendo wa Kusebeneka mpaka kieleweke kwa mashabiki na wapenzi wa Skylight Band
Ni happy mwanzo mwisho kwa mashabiki wa Skylight.
Mmoja wa mashabiki wa Skylight band akiogeshwa kwa vinywaji wakati wa kusherekea siku yake ya kuzaliwa kwenye kiota hiki cha Thai Village wakati band ya Skylight ikiendelea kutoa burudani
Ni mwendo wa Nigerian Flava ni noma sana karibu leo ujione mwenyewe usisubirie kuadithiwa
Kumbukumbu zikichukuliwa hapa tunaweza kusema mpiga picha kapigwa picha
John Music (katikati) akitoa burudani kwa wapenzi na mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) Ijumaa iliyopita huku akipewa sapoti ya waimbaji wenzake wa Skylight Band.
Wakati Sam Mapenzi akiimba wimbo wa "All of Me" mdada huyu ulimgusa sana mpaka akashindwa kujizuia akaamua afanye ya kwake
Mdada akichukua selfie na msanii wa Skylight Band Sum Mapenzi baada ya kumkuna na weimbo wa "All of Me"

No comments:

Post a Comment