Pages

Wednesday, April 15, 2015

TAZAMA PICHA INAVYODAIWA MCHEZAJI WA REAL MADRID ALIMNG'ATA MSHAMBULIAJI WA ATLETICO

Na Anwar Binde.
Mlinzi wa pembeni wa Real Madrid Dani Carvajal amekataa tuhuma za kumn’gata mshambuliaji wa Atletico Madrid Mario Mandzukic wakati wa mchezo wao wa robo fainali ligi ya mabingwa uliofanyika jana jumanne. Vyombo mbalimbali wa habari nchini Hispania wanamtuhumu carvajal kumn’gata na kiwiko halafu kumtandika ngumi maneo ya tumboni ilionyesha kipande cha video toka Vicente Calderon.
Mandzukic alihusishwa katika matukio mengi ya 


vurugu dhidi ya Real,pia mshambuliaji huyo toka taifa la Croatia pia alipata majanga mengine baada ya kupigwa kiwiko na mlinzi wa Real Sergio Ramos na kumpasua sehemu ya puani iliyompelekea kuvuja damu na kupata matibabu.
Lakini Carvalaj alipinga kufanya tukio hilo,“niliona baada ya mchezo kuisha kwamba natuhumiwa kumn’gata mpinzani wangu”aliandika kwenye mtandao wake wa twitter.

Kocha wa Atletico Diego Simione aliulizwa kuhusu tukio wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mchezo kuisha alisema “sikuliona tukio hilo na siwezi kusema lolote”.

Kocha huyo raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 44 aliongeza kuwa kiwiko alichopigwa Mandzukic na mlinzi Ramos ilikua ni bahati mbaya.

No comments:

Post a Comment