Pages

Monday, April 27, 2015

TAZAMA PICHA::VIJANA WANAODAIWA KUWA WANACHAMA WA CHADEMA WAKAMATWA NA VIFAA MBALI MBALI VYA UJAMBAZI

Baada ya mkuu wa jeshi la polisi nchini kuvipiga marufuku vyama vyote vya siasa kuwa na makundi ya kujihami katika vyama hivyo, CHADEMA wamekaidi agizo hilo halali la polisi na wameendelea kuwatumia Red Brigedi katika chama chao. 
Zifuatazo ni picha za vifaa vya kijambazi vilivyonaswa na jeshi la polisi.
Mnamo tarehe 24/4/2015 huko maeneo ya Sogea Tunduma Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, METHEUS ANGANILE MWAFONGO, Mndali, 37yrs, Mkuu wa Ulinzi CDM Wilaya Momba, pamoja SALEHE TABLEI@SICHALWE, 22yrs, mkazi wa Majengo Tunduma walikamatwa kutokana na taarifa za kiintelijensia.

Watu hawa walikamatwa wakiwa na buti pair 2 za kijeshi, kofia pair 2 za kijeshi, kamba kurukia ya mazoezi, vyuma kwa ajili ya mazoezi ya pushup, visu pair 2 kimoja spring knife na kingine kisu kikubwa, miwani ya FFU(ya kwenye misafara), manati pair 2 na mawe yake 40 pamoja na nati 4 zilizotarajiwa kutumiwa kama mawe, shenguard kwa ajili ya mikono na miguu pair 4, Bendera 2 za CDM, Tshirt 1 ya CDM, Kilemba 1, koti 1, Pamoja na barua 3 za CDM za kata ya MSANGANO, SHITETE, na KAMSAMBA (W) MOMBA zenye kichwa cha habari "UTOAJI WA VIONGOZI WA RED BRIGED KATIKA KATA YENU KWA MAFUNZO YA RED BRIGED".
Barua inasomeka hivi
Husika na kichwacha barua hapo juu chajifafanua vema.
Napenda kukujulisha kuwa kutakuwa na ziara ya kimafunzo ya RB (Red Briged) katika kata yenu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
Na kwa barua hii naomba uwapokee na uwape ushilikiano wa kutosha kwa ajili ya maendeleo ya chama chetu.
Ni matumaini yangu kuwa utawapokea na kuwatunza pamoja na usalama wao.
Wako katibu wa chama Wilaya.

Katika mahojiano vijana hawa walikuwa wakienda kutoa mafunzo ya kijeshi katika kata tajwa na mpango wao ni kufundisha vijana 300 katika wilaya ya Momba na mpango huu ni wa mkoa na Nchi nzima chini ya Mkurugenzi wa Usalama Taifa CDM bwana LWAKATARE.



No comments:

Post a Comment