Siku moja baada ya kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi, Nepal imeshuhudia tetemeko lingine kubwa lililoelezewa kusababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kathmandu.
Maofisa nchini humo wamesema kuwa vikosi vya uokoaji vinaendelea na kazi ya kuwatafuta watu walionusurika, na wanahofu kuwa idadi ya watu waliofariki dunia inaweza kuongezeka.
Tetemeko hilo pia limeleta madhara katika nchi jirani za India inakoripotiwa kuwa watu 53 wamefariki dunia, 17 Tibeti na 4 Bangladesh.
Pia tetemeko hilo limesababisha maporomoko katika milima Everest ambapo watu 18 wamefariki dunia na kujeruhi wapanda mlima huo wengine 30.
Wananchi wakiwa wamekusanyika katika maeneo ya wazi mitaani mjini Kathmandu baada ya kutokea kwa tetemeko hilo.
No comments:
Post a Comment