Watu 10 wamekufa katika ajali
iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mkata katika Kijiji cha Mbweni
Wilayani Handeni Mkoani Tanga majira ya saa 5 asubuhi ya leo.
Polisi mkoani Tanga
wamethibitisha tukio hilo na kusema ajali hiyo imehusisha mabasi mawili ya
abiria na gari dogo katika barabara ya Dar es Salaam kwenda Tanga na Arusha.
Kwa mujibu wa Jeshi hilo gari dogo ilikuwa likitaka kulipita
lori lililokua mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la RATCO
lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dar es Salaam.
Baada ya Basi la
RATCO kugonganana na gari dogo, lilipoteza mwelekeo na kugongana tena uso kwa
uso na basi la Kampuni ya Ngolika lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda
jijini Arusha.
Kati ya watu 10
waliokufa wanaume ni watano akiwemo Dereva wa gari dogo na Dereva wa basi la
Kampuni ya Ngorika pamoja na wanawake watano wakiwemo watoto wawili.
Mpaka sasa
maiti kumi zimeshatolewa huku jitihada zaidi zikiendelea kujua kama bado wapo
ambao wamo ndani ya magari hayo yaliyogongana uso kwa uso au laa.
Picha hizi ni
kwa hisani ya Mtandao wa Mabalozi wa Usalama barabarani Tanzania (RSA).
No comments:
Post a Comment