Dar es Salaam. Kiongozi wa Chama cha
ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema atalazimika kuachia wadhifa huo kwa
mtu mwingine atakayeteuliwa na chama hicho kugombea urais katika
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Kwa mujibu wa katiba ya chama hicho mwanachama
anayeruhusiwa kugombea urais ni lazima awe kiongozi wa chama, wadhifa
ambao unashikiliwa na Zitto ambaye hajafikisha umri wa kikatiba wa
kugombea urais ambao ni kuanzia miaka 40. Kwa sasa ana miaka 39.
kugombea urais ambao ni kuanzia miaka 40. Kwa sasa ana miaka 39.
Zitto alitoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari wa Mwananchi katika ofisi za gazeti hili Dar es Salaam juzi.
“Ikitokea hivyo (ACT ikapata mgombea urais, kutoka
ndani au nje ya chama hicho), mimi natoka namwachia mtu mwingine na
tumeshaamua hivyo, kwetu sisi tatizo siyo cheo. Tukipata mgombea urais
leo nitampisha, sitakuwa kiongozi wa chama nitabaki kuwa mwanachama wa
kawaida na mjumbe wa Kamati Kuu.”
Hata hivyo, alisema ili mtu huyo apate nafasi hiyo
ni lazima aelewe malengo ya chama hicho kilichopata usajili wa kudumu
Mei, mwaka jana.
“Tunataka mtu ambaye hata tukipata mabadiliko
asiwe kikwazo cha hayo mabadiliko. Nasema hivi kwa sababu mnaweza kupata
mtu mwingine kuwa kiongozi wa chama lakini baadaye anang’ang’ania na
hataki kutoka,” alisema.
Alifafanua kuwa yeye bado ni kijana ana muda mrefu
katika siasa na anaungwa mkono sehemu nyingi, hivyo hana haja ya
kuharakisha katika kila jambo.
Hata hivyo, akizungumzia watu wa vyama vingine
watakaojiunga na chama hicho alisema, “Kati ya watu watakaojiunga ACT au
walioonyesha nia kutoka CCM au Ukawa hadi sasa hakuna ambaye ni mgombea
urais.”
Alifafanua, “Sisi (ACT) tutasimamisha mgombea wetu
wenyewe katika nafasi ya urais au tunaweza kumuunga mkono mgombea wa
upinzani.”
Alisema watafanya hivyo kwa sababu hawataki kuua
matumaini ya nchi kupata Serikali inayotokana na vyama vya upinzani,
“Pale ambapo tutaona ni lazima kuunga mkono wenzetu kuing’oa CCM
madarakani tutafanya hivyo. Si kama tunajiunga Ukawa, hapana ni kwa
sababu bado hatujawa na mazungumzo nao na kujua nini
kitakachotuunganisha.”
Sera na Ilani
Zitto aliziponda sera na ilani za vyama vya siasa
nchini kwamba hazina tofauti, zote zina mfumo wa kiitikadi na mwelekeo
uleule, isipokuwa kwa ACT Wazalendo
- Mwananchi
No comments:
Post a Comment