Kamanda
wa Polisi Dodoma DAVID MISIME - SACP akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) baada ya kuwakamata wezi watatu kutokana na wizi
waliokuwa wakiendelea kuufanya mkoani Dodoma.
Baadhi
ya laptop zilizoibiwa kwenye sehemu mbalimbali mkoani Dodoma
zikioneshwa kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) mara baada ya
kukamatwa wezi hao.
Hivi ni vifaa vya kuvunjia vilivyokamatwa na jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma
Baadhi ya mabegi yaliyokuwa yametunza laptop pamoja na vifaa vilivyokuwa vinatumika kuibia
Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyekamatwa katika
nyumba ya kulala wageni iitwayo Yarabi Salama (Yarabi Salama guest
house) katika Manispaa ya Dodoma. Aliyekamatwa anafahamika kwa jina la
MASAGARA S/O MESO, Mwenye miaka 40, Kabila Mzanaki wa Butihama, akiwa na
funguo bandia 19, Master key 2, Bisibisi 2, Kisu kimoja, Tupa moja,
Mikasi mitatu mikubwa ya kukatia vyuma, Msumeno ya kukatia vyuma mitano,
Mitalimbo ya kuvunjia miwili, Adjustable spanner 1, Kipande cha bomba,
Biti za kutobolea vyuma na mbao 8, Simu mbili aina ya Tecno na Nokia,
Simu ya bandia ya Nokia, Pochi za mfukoni mbili, Hati ya dharura ya
kusafiria, Betri ya simu moja, Nyenzo moja ya mbao, Nguo za kubadilisha,
Madawa mbalimbali ya kienyeji, Kipande cha nondo kimoja na Irizi moja
aliyokuwa amefunga sehemu ya juu ya mkono wa kushoto akiwa amehifadhi
kwenye begi lake kwa maandalizi ya kufungua vyumba vya wapangaji wengine
na kuvunja mita ili aibe.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME – SACP amesema baada ya mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri
kufanya uhalifu wa kuvunja nyumba mbalimbali za kulala wageni na
kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu huko Mikoa ya Mwanza, Geita,
Shinyanga, Tabora na hapa Dodoma. Uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini
watuhumiwa wengine anaoshirikiana nao pamoja na matukio aliyofanya.
Kamanda
MISIME amesema nimuhimu kwa wenye nyumba za kulala wageni kuwa makini
na wageni wanaowapokea kwani baadhi yao wanapanga vyumba kwa lengo la
kufanya uhalifu wa kuwaibia wateja wengine au vifaa vya hoteli kama TV,
DVD Player, Ving’amuzi n.k na wakati mwengine hufanya vitendo vya wizi
mitaani.
Pia
Kamanda MISIME amesema katika hatua nyingine Jeshi hilo linamshikilia
ONESMO S/O LUPILI YEYO Mwenye miaka 22, Muha, Mwenyeji wa Mkoa wa mwanza
ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Kitivo cha
Sayansi ya Jamii mwenye namba za usajli T/UDOM/2013/01760 kozi ya
Uhasibu mwaka wa kwanza ambaye alisimamishwa masomo baada ya kukosa sifa
ya kuendelea na masomo chuoni hapo. Baada ya wanafunzi kulalamika mara
kwa mara kuibiwa mali zao ndipo tulipofanikiwa kumkamata.
Mtuhumiwa
huyo baada ya kuhojiwa alikiri kufanya uhalifu wa uvunjaji na wizi wa
laptop na simu, alieleza kuwa mpaka anakamatwa na kuhojiwa alikuwa
ameshaiba laptop zaidi ya 40 pamoja na simu zaidi ya 80 chuoni hapo.
Kamanda
MISIME ameendelea kusema kuwa baada ya ufuatiliaji katika kumbukumbu za
Polisi, jumla ya matukio 30 yameripotiwa katika kituo cha Polisi UDOM
na jumla ya Laptop zinazokadiriwa kuwa zaidi ya 60 zimeibiwa katika
vitivo mbalimbali ndani ya chuo hicho ikiwemo kitivo cha Sayansi ya
Jamii na Elimu.
Mtuhumiwa
huyo alipohojiwa zaidi alikwenda kuonyesha kwa mtu aliyemuuzia vitu
hivyo baada ya kuiba, mtu huyo alibainika kuwa ni ISSACK S/O LEMA Mwenye
miaka 29, Mkazi wa Airport ambaye ni fundi wa kutengeneza komputa
maeneo ya Mtendeni Street Dodoma pembeni ya jingo la Bima.
Polisi
walifika kwa mtu huyo na alipohojiwa alikiri kupokea Laptop zaidi ya 19
kutoka kwa mtuhumiwa ONESMO na imebainika fundi huyu mara baada ya
kuletewa laptop na mtuhumiwa anazifungua na kuuza kifaa kimoja kimoja.
Kamanda
MISIME ametoa wito kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbli kuwa makini na
baadhi ya wanafunzi waliosimamishwa na kufukuzwa chuo kwani imebainika
ndio wanaoshikiana na wahalifu wengine kuiba vitu mbalimbali katika
vyuo, pia wananchi nao wasinunue vitu bila ya kupewa risiti au
kuandikishiana kwa mujibu wa sheria ili kujenga uaminifu kwa anayenunua
na anayeuza mali la sivyo unaweza kushitakiwa kwa kukutwa au kupokea
mali ya wizi.
No comments:
Post a Comment