Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, May 21, 2015

HII NDIO REKODI YA KOCHA WA TAIFA STARS NOOIJ

Na Berthar Lumala
TAIFA Stars imeaga rasmi michuano ya Cosafa baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Mdagascar kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng jijini Rustenburg, Afrika Kusini.
Kipigo hicho kimeendeleza rekodi mbaya ya Nooij ambaye tangu aanze kuinoa Stars ikiwa ni mechi ya 15 , ameshinda tatu, sare sita na vipigo sita.
Nooij alirithi mikoba ya Mdenmark Kim Poulsen aliyetimuliwa bila sababu za msingi.Baada ya mechi hiyo kumalizika, Nooij amesema: "Kikubwa si 



matokeo, tunaandaa timu ya kuikabili Uganda katika michuano ya CHAN na Misri katika mashindano ya AFCON.(P.T)Matokeo hayo yameifanya Madagascar kufikisha pointi sita baada ya kushinda 2-1 dhidi ya Lesotho katika mechi ya kwanza ya Kundi B iliyochezwa Jumatatu wakati Stars ililala 1-0 dhidi ya Swaziland.

Madagascar walienda mapumziko wakiongoza kwa mabao mawili yaliyofungwa na winga wa kushoto Njiva Rakotoarimalala na mshabuliaji Rhino Randriamamaka.
Bao la kwanza limetokana na shambulizi la kushtukiza winga huyo alipotumia fursa ya makosa ya kujisahau na kujichanganya kwa mabeki wa Stars waliompa nafasi mfungaji kutuliza mpira kisha kumtungua kwa shuti kali la mguu wa kulia kipa Deogratius Munishi 'Dida' katika dakika ya 13.
Randriamamaka akafuta ndoto za Watanzania kushinda baada ya kufumua shuti kali la mguu wa kulia lililobabatiza vidole vya Dida akimalizia kwa ufundi kazi nzuri ya mfungaji wa bao la kwanza, Rakotoarimalala ambaye aliwapiga chenga mabeki wa Stars na kupenyeza pasi ya kisigino kwa mshambuliaji huyo.
Kipindi cha pili kocha wa Stars, Mart Nooij, aliwatoa winga Mrisho Ngasa, mshambuiliaji Juma Liuzio na kiungo Said Ndemla kisha nafasi zao kuchukuliwa na winga Simon Msuva, beki Shomari Kapombe na mshambuliaji Ibrahim Ajibu, mabadiliko ambayo hayakuisaidia timu yake kupata bao hata moja dhidi ya timu hiyo iliyopo nafasi ya 150 katika viwango vya FIFA kwa sasa.

Kikosi cha Taifa Stars kilianza na Deogratius Munishi, Erasto Nyoni, Oscar Joshua, Aggrey Morris, Salum Mbonde, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Said Hamis Ndemla/ Shomari Kapombe, John Bocco, Juma Luizio/ Ibrahim Ajibu na Mrisho Ngassa/ Simon Msuva (dk 46).

No comments:

Post a Comment