Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewafuta kazi mawaziri
watatu, huku maandamano yakiendelea katika mji mkuu kufuatia jaribio la
mapinduzi, juma lililopita.
Mawaziri walioachishwa kazi ni wa Ulinzi, mashauri ya nchi
za kigeni na biashara.
Mapema hii leo, polisi walifyatua risasi hewani katika mji
mkuu Bujumbura, kujaribu kuutawanya umati wa vijana uliokuwa ukifanya ghasia.
No comments:
Post a Comment