Pages

Monday, May 18, 2015

TAKWIMU ZAKWAMISHA UPATIKANAJI WA MAENDELEO

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Bi Amina Shabani akifungua semina ya siku moja ya kujadili mpango utekelezaji wa Maendeleo ya Malengo ya Millenia MDG’s, iliyofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar na kuwashirikisha Maofisa Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Viongozi wa Taasisi zisizo za Kiserekali, ulioandaliwa na Tume ya Mipango Zanzibar na Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania na
 kufadhiliwa na UNDP. Na Mwandishi wetu, Zanzibar UKOSEFU wa takwimu sahihi katika masuala mbalimbali umeelezwa kuchangia kutopiga hatua kwenye mipango ya kimaendeleo inayopangwa na serikali juu ya wananchi. Aidha upotoshaji wa takwimu hizo unaofanywa na baadhi ya watendaji kwa kutaka kujinufaisha wao wenyewe pia umekuwa ukichangia kuchelewa hatua za kimaendeleo. Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Zanzibar, Amina Shaaban wakati akifungua semina ya siku moja ya kujadili Malengo ya Millenia baada ya 2015 iliyofanyika mjini hapa. Amina alisema, kuwa takwimu ndiyo zinaonesha hali halisi na pia zinawezesha fedha kutoka kulingana na mahitaji, hivyo ni muhimu kuzingatiwa kwa jambo hilo ili mipango ya maendelo iweze kufanyika kwa wakati. "Kulikuwa na kamati ile ya ufundi na ya muda, siku hizi hazipo kama zimekufa ni vyema zikarudishwe tena maana zilikuwa na jukumu la ufuatiliaji na kutukumbusha mara kwa mara," alisema Amina. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi (ESRF), Dk. Oswald Mashindano alisema, semina hiyo inalenga kujadaili utekelezaji wa malengo ya millenia kabla ya kumalizika Septemba, mwaka huu na ajenda mpya ya maendeleo baada ya Septemba, mwaka huu. Aidha alisema, nchi nyingi hazijakuwa na uwezo wa kutekeleza malengo ya millenia ikiwemo Tanzania, hivyo kutokana na hali hiyo ilikubalika kuwepo kwa ajenda mpya ya maendeleo baada ya Septemba, mwaka huu. "Kwa sisi Tanzania kidogo tuna bahati ya kuiga hatua kidogo, lakini pamoja na kutimiza baadhi ya malengo, bado kuna maeneo ambayo hatujafanikiwa sana na moja kati ya sababu iliyofanya tukwame ni pamoja na ukuaji wetu wa uchumi," alisema. Akizungumzia kuhusu kamati za ufundi na ya muda, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kiamatifa wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy alisema, kuwa suala hilo atalirudisha kwenye tume ya mipango ya Tanzania Bara ili liweze kushughulikiwa kwa wakati. Hata hivyo alisema, ili nchi iweze kupiga hatua katika mikakati ya maendeleo ni muhimu kwa sekta binafsi kushiriki kwa mstari wa mbele kutokana na kuwa nafasi kubwa katika kuendeleza maendeleo na uchumi wa taifa. "Sekta binafsi wao ndiyo wenye pesa nyingi sana kuliko serikali, ukiangalia hata katika nchi zilizoendelea sekta binafsi kwa kiasi kikubwa zimechangia sehemu kubwa ya maendeleo yao," alisema Balozi Mushy. Balozi Mushy alisisitiza umuhimu wa takwimu sahihi kwa kuwa ndiyo silaha pekee katika kufanikisha mipango ya kimaendeleo kukamilika kwa wakati. Semina hiyo iliwashirikisha wataalamu wa tume ya mipango ya Zanzibar na 

 
tasisi zingine za serikali ilikuwa inalenga kuwajengea uwezo na kujadili ajenda 17 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na mipango ya maendeleo baada ya kukamilika kwa Malengo ya Maendeleo ya Millenia (MDGs) Septemba, mwaka huu.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia hutuba ya Katibu Mtendaji Bi Amina Shabani akifungua mkutano huo.
Mwakilishi wa UN Zanzibar Bi. Anna Senga akitoa salamu za Umoja wa Mataifa (UN) wakati wa mkutano wa kupitia mafanikio ya Maendeleo ya Malengo ya Millenia MDG's.
Washiriki wakiwa katika ukumbi wa Mkutano hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar. wakifuatilia mada zinazotolewa wakati wa mkutano huo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi (ESRF), Dk Oswald Mashindano akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kupitia mafanikio ya Maendeleo ya Malengo ya Millenia MDG's Tanzania uliofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Washiriki wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakifuatilia kwa utulivu michango na mada zilizoku zikiwasilishwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano Wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akiwasilisha mada jinsi mataifa yalivyofikia SDGs, michakato inayoendelea na namna ambavyo Tanzania inaweza kunufaika na mkakati mzima wa maendeleo.
Balozi Celestine Mushy akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo .
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi (ESRF), Dk Oswald Mashindano akiwasilisha mada ya "Elucidating SDG 17 on means of implementation and Global Partnership for Development and Financing of Post MDG's Development Agenda".
Washiriki wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakifuatilia mada zinazowasilishwa na wahusika.
Dk. Kenneth Mdadila, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam Idara ya Uchumi akiwasilisha mada ya "Tanzania's preparedness in Monitoring Sustainable Development Goals- Analysis Based on Global Indicator Framework" katika semina hiyo..
Pichani juu na chini ni washiriki wa semina ya siku moja ya kujadili Malengo ya Millenia baada ya 2015 iliyofanyika mwishoni mwa wiki visiwani Zanzibar.
Pichani juu na chini ni Maofisa mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa taasisi zisizo za Kiserikali wakishiriki kuchangia mada katika semina hiyo ya siku moja iliyofadhiliwa na UNDP.
Mdau Yasser Manu kutoka ESRF.
Washiriki wakichangia mada zilizowakilishwa wakati wa semina ya siku moja iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment