Baraza
la vijana wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema limewataka
wananchi wasidanganyike na viongozi wanaotumia nguvu kupata madaraka
badala yake wapime viongozi waadilifu na wazalendo kwa taifa waliotayari
kubadilisha maisha ya watanzania walio wengi na si kujinufaisha
wenyewe.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa ifakara
wilayani kilombero katibu mkuu
wa baraza la vijana wa Chadema taifa Julius Mwita amewataka wananchi kujiandikisha katiba daftari la wapiga kura ili watumie fursa kwenye sanduku la kura kuchagua viongozi wazalendo na si viongozi wenye nia ya kujinufaisha.

Naye katibu mwenezi wa baraza hilo Edward Simbeye amesema
inashangaza kuona vigogo wanatumia gharama kubwa kutangaza nia ya
kugombea urais huku wananchi wakikosa huduma za afya ambapo amewashauri
wakazi wa Ifakara kufanya uamuzi mgumu kwa kuchagua viongozi wa Ukawa
mwezi Oktoba mwaka huu watakaosaidia kuleta mabadiliko ya kiuchumi
katika jamii.
No comments:
Post a Comment