Wenyeji Chile wametinga hatua ya fainali ya Copa America baada ya kuifunga timu pungufu ya Peru magoli 2-1 katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa usiku wa kuamkia leo mjini Santiago.
Eduardo Vargas ameifungia Chile magoli mawili katika dakika ya 42' na 64', lakini dakika ya 60' Mlinzi Gary Medel alijifunga bao na kuwapa angalau ahueni Peru.
Mapema dakika 20' Mwamuzi wa mechi, Jorge Argote alimuonesha kadi nyekundu (Umeme) Carlos Zambrano kwa kosa la kumkanyaga mgongoni kiungo wa Chile,Charles Aranguiz.
Chile watacheza fainali na Argentina au Paraguay ambao wanakutana leo majira ya saa nane na nusu usiku kwa saa za Afrika Mashariki katika mechi ya pili ya nusu fainali.
No comments:
Post a Comment