Staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond STAA wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul
‘Diamond Plutnumz’ ambaye aliwatelekeza watoto wawili alioahidi
kuwasomesha katika shule ya East Africa International ya Mikocheni
jijini Dar es Salaam, atashtakiwa mahakamani endapo wazazi wa vijana hao
wataamua kufanya hivyo, Risasi Mchanganyiko limeelezwa.tnumz’.
Meneja wa msanii huyo, Babu Tale, awali aliulizwa na gazeti hili juu
ya kinachoendelea kuhusiana na vijana hao waliotimuliwa shule Aprili
mwaka huu kwa kutolipiwa ada, lakini akionekana kupatwa na jazba,
alisema wanasikitishwa na jinsi wazazi wa watoto hao wanavyokiuka
makubaliano, hivyo wao hawataki tena kusema lolote kwa sasa.
“Kama wao wanadhani kwa kwenda kwenye media (vyombo vya habari) ndiyo
watoto wao watasomeshwa, basi na waende hukohuko watasomeshewa watoto
wao,” alisema Tale aliyeonekana kukasirishwa na mwendelezo wa habari
hiyo.
Tale alitoa kauli hiyo kufuatia mmoja wa wazazi hao wa watoto Hillary
na Hamis, kudai kuwa hakuna maendeleo yoyote ya kulipiwa ada kwa vijana
wao, kwani ingawa waliambiwa mambo yangekuwa sawa baada ya siku chache,
lakini danadana zinaendelea.
Mwanasheria mmoja maarufu nchini aliyeomba hifadhi ya jina lake,
aliliambia gazeti hili kuwa endapo wazazi wa vijana hao wataamua, sheria
zinawaruhusu kumpeleka mahakamani msanii huyo kwa kukiuka mkataba, hata
kama haukuandikwa.
“Makubaliano ya mdomo ni mkataba unaotambuliwa kisheria, mradi tu
wazazi waweze kuthibitisha, tena kwa hili, inaonyesha siyo tu mkataba,
bali inaonyesha Diamond hakufanya hivyo kwa mapenzi yake kwa watoto,
bali baada ya wao kumfanyia kitu, aliwapeleka shule kuonyesha u-siriazi
aliokuwa nao juu ya ahadi hiyo,” alisema mwanasheria huyo.
Januari mwaka jana, Diamond aliendesha shindano kwa watoto la kucheza
mtindo wa Ngololo na kuahidi zawadi kwa washindi katika Viwanja vya
Leaders Club, Kinondoni, Dar. Vijana hao walioshinda, walipewa ofa ya
kusomeshwa katika shule hiyo hadi kumaliza elimu yao ya msingi, lakini
tangu wapelekwe hawajawahi kulipiwa ada.
No comments:
Post a Comment