Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, June 4, 2015

Mfuko wa Pensheni wa PSPF Wakabidhi Msaada kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar.‏

 
Ofisa wa Mfuko wa Pensheni PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akimkabidhi msaada wa Magogoro Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ame Perera kwa ajili ya Wananchi waliopata maafa ya mvua na kuharibikiwa na mali zao, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda ya ngome chumbini Zanzibar.


 OFISA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akitowa maelezo kwa niaba ya Mkufugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi msaada wa Magodoro kwa wananchi wa Jimbo la Chumbuni waliopata janga la mvua za masika katika shehia tatu za jimbo hilo, Chumbuni. Karakana na Muembemakumbi Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Perera Ame Silima akitowa shukrani kwa uongozi wa Mfuko wa PSPF kwa msaada wao kwa Wananchi wa Jimbo lake wakati wa makabidhiano hayo yaliofanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda ya ngombe chumbuni Zanzibar.Mhe Mbunge akiishukuru PSPF kwa kutumia sehemu ya pato lake kwa kusaidia Jamii.
Sheha wa Shehia ya Karakana Ndg Bakari Makame akitowa shukrani kwa niaba ya wananchi wake kwa Msaada wa Magodoro yaliotolewa na Mfuko wa PSPF kwa kujali wananchi wakati wa maafa  na kutowa shukara hizo kwa Uongiozi huo wakati wa makabidhiano ya msaada huo yaliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Mabanda ya Ngome Chumbuni Zanzibar.
  WANANCHI wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya mvua hivi karibuni.
Wananchi wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakimsikiliza Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa maelezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata maafa ya mvua hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment