Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, June 1, 2015

MKE WA WAZIRI MKUU AZINDUA TAASISI YA MANJANO FOUNDATION‏

Mgeni Rasmi kwenye halfa ua Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Pamoja na Vipodozi Pendwa Vijulikanavyo kama Luv Touch Manjano Mke wa Waziri Mkuu Mh Tunu Pinda Akitoa Hotuba yake katika Uzinduzi huo .Katika Hotuba yake Mh Mama Pinda Alisema amefurahishwa sana Kwa Mwanamke wa Kitanzania Kuanzisha Bidhaa amabyo imeweza kushindana na Bidhaa kama hizo kutoka mataifa Mengine.Halfa hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.Hafla hiyo ya uzinduzi ilifunguliwa na mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania mama Tunu Pinda. Alizindua rasmi kwa soko la Tanzania poda ya luvtouch Manjano, rangi ya awali (foundation), na rangi ya mdomo (lipstick) na walio hudhuria hafla hiyo walipata nafashi ya kushuhudia thamani ya bidhaa hizo, aina ya urembo na viwango vya ubora vinvyoshinda hoja zote na kuthibitisha kuwa bidhaa za hapa nchini zinaweza kushindana na bidhaa za kimataifa. Wanawake wengi walipata fursa ya kujaribu moja ya bidhaa hizo na waliweza kununua bidhaa za LuvTouch Manjano ukumbini.

Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar Akisisitiza Jambo kwenye Halfa Hiyo.Mh Balozi Majaar Alisisitiza Umuhimu wa Kumsomesha Mtoto wa Kike Pamoja na Kuwawezesha Kiuchumi.Balozi Majari alisiistiza Jamii ya Kitanzania Kuachana na Kasumba ya Kuwanyanyapaa Watoto wa Kila pia Kutokuwawezesha na Akasema mtoto wa Kike akipewa Fursa ya Kupata Elimu na Kuwezeshwa Wanawake Wanaweza .


Hafla hiyo pia ilihusisha kuzindua Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Shirika hili limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu. Shear illusions ilikusanya wanawake takriban 450 wa Kitanzania kusherehekea miaka 10 ya safari ya kumfurahisha kila mwanamke, pamoja na kuzindua kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano iliyobuniwa na Shekha Nasser, mmiliki wa Shear illusions. Pamoja na uzinduzi huo, alizundua pia kitabu cha muongoza kwa kina mama kuonyesha jinsi ya kujipodoa kitaalam kwa kutumia nyenzo na vipodozi sahihi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Katikati akiongea Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda (Kulia) Pamoja na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar
Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul Wakati wa Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Pamoja na Uzinduzi wa Vipodozi Pendwa vya Luv Touch.
Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul (Kulia) Akiwa n Mtoa Mada katika Halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda
Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi akitoa Burudani ya aina yake kwenye Halfa hiyo iliambatana na Uzinduzi wa Vipodozi vya Luv Touch 
Wageni waalikwa walioshiriki katika halfa ya Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation
Mshereheshaji wa Halfa Hiyo Ndugu Angela Bongo akiwa na Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser wa Pili Kushoto akiwa Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda wa Pili Kulia Pamoja na Watoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar na Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda.
Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda Katikati Pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser wa Kushoto na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda. 
wageni walikwa




No comments:

Post a Comment