WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya,
ameonya wanaojadili wengine badala ya hoja katika kipindi hiki cha
kuelekea uchaguzi mkuu kuwa hawawezi kuisaidia nchi kwa mtindo huo.
Profesa Mwandosya alisema hayo mjini hapa jana, alipokuwa akitafuta
wadhamini ambao CCM imewataka kwa mtu anayetangaza nia ya kugombea urais
na kuchukua fomu.
Kwa mujibu wa matakwa ya chama hicho, anayetangaza nia na kuchukua
fomu za kugombea nafasi hiyo anapaswa kutafuta wadhamini 450 kutoka
mikoa 15 ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Alisema ukiona mtu anaacha hoja ya msingi na kuanza kumjadili mtu, ujue kuwa hana busara na hajakomaa kisiasa.
Kwa maelezo ya Profesa Mwandosya, wanaotangaza nia wanapaswa
kuwaeleza wananchi jinsi watakavyotatua kero zao na kuwaletea maendeleo,
hivyo suala la msingi la kujadiliwa linafaa kuwa hoja za mtangaza nia,
kuona endapo zina mantiki au la.
No comments:
Post a Comment